IQNA

Wasiwasi wa Umoja wa Mataifa kuhusu Israel kuwafunga Wanaharakati Wapalestina

14:39 - August 13, 2021
Habari ID: 3474187
TEHRAN (IQNA)- Afisa mwandamizi wa Umoja wa Mataifa amebainisha wasiwasi wake juu ya kampeni ya utawala wa Israeli ya kuwakamata, kuwatesa na kuwakandamiza watetezi wa haki za binadamu wa Palestina kote Ukingo wa Magharibi unaokaliwa kwa mabavu na utawala huo.

"Kukamatwa na uvamizi wa nyumba za watetezi wa haki za binadamu wa Palestina [na vikosi vya jeshi la Israeli] ni sehemu ya ukandamizaji mkubwa dhidi ya wale wanaotetea haki za binadamu za Wapalestina katika Ardhi za  Palestina zinazokaliwa kwa mabavu," Ripota Maalumwa wa UN kuhusu hali ya watetezi wa haki za binadamu, Mary Lawlor, alisema.

Lawlor pia alikosoa kukamatwa na kuwekwa kizuizini  kwa wakili wa Palestina na mtetezi wa haki za binadamu Farid Al-Atrash, ambaye pia ni mkurugenzi wa ofisi ya Tume Huru ya Haki za Binadamu (ICHR) kusini mwa Ukingo wa Magharibi.

Vikosi vya jeshi la Israeli viliweka kizuizini Al-Atrash baada ya kushiriki maandamano ya amani katikati mwa Ukingo wa Magharibi mwa mji wa Beit Lahm (Bethlehem), ulio kilomita 10 (maili 6.2) kusini mwa al-Quds (Jerusalem) mnamo Juni 15 na kuachiliwa kwa dhamana siku nane baadaye.

Mtaalamu huyo wa UN pia alielezea wasiwasi wake juu ya uhamisho wa lazima wa Wapalestina wanaoishi katika maeneo ya Sheikh Jarrah na Silwan ya al-Quds.

Sheikh Jarrah limegeuka na kuwa eneo la ukandamizaji wa mara kwa mara wa polisi wa Israel kwa Wapalestina wanaoandamana kupinga kufurushwa kwa familia kadhaa za Wapalestina kutoka kwa nyumba zao kwa ambazo zinatekwa na magenge ya walowezi wa Kizayuni wanaopata himaya ya Israel.

3475481

captcha