IQNA

Wafanyaziara takribani milioni sita washiriki maombolezo ya Imam Hussein AS huko Karbala, Iraq

12:57 - August 20, 2021
Habari ID: 3474209
TEHRAN (IQNA)- Naibu Mkuu wa mkoa wa Karbala nchini Iraq ametangaza kuwa mazuwari takribani milioni sita wamehiriki katika maombolezo ya Imam Hussein AS yaliyofanyika katika Siku ya Ashura hapo jana kwenye mji huo mtakatifu.

Jasim Al Fatlawi, Naibu Mkuu wa Mkoa wa Karbala ametangaza kuwa, mji huo mtakatifu jana ulipokea wafanyaziara karibu milioni sita, wakiwemo elfu tano kutoka nje ya Iraq.

Jeshi la kujitolea la wananchi wa Iraq, Al Hashdu-Sha'abi lilikuwa limetoa taarifa hapo kabla kuwa, zaidi ya wanachama elfu saba wa jeshi hilo wameshiriki katika mpango maalum wa kudhamini usalama katika hafla ya maombolezo ya Ashura.

Jana Alkhamisi ya tarehe 10 Mfunguo Nne Muharram 1443 Hijria ilisadifiana na Ashura ya Imam Hussein AS.

Waombolezaji wa Ashura hukusanyika katika siku hii na kushiriki kwenye majlisi na hafla za maombolezo kila pembe ya dunia kuadhimisha kuuawa shahidi kwa Imam Hussein (as), Imamu wa Tatu wa Waislamu wa madhehebu ya Shia pamoja na wafuasi wake waaminifu.

Licha ya kupita karne nyingi tangu lilipotokea tukio chungu la kuhuzunisha na kuungulisha nyoyo la Karbala na kuuawa shahidi kidhulma na kikatili Imam Hussein (as) na wafuasi wake waaminifu, si tu hadhi na umuhimu wa tukio hilo haujapungua, lakini kadiri siku zinavyopita ndivyo ujumbe wa Ashura unavyozidi kusambaa na hafla za maombolezo ya tukio hilo kufanyika kwa msisimko na uelewa mkubwa zaidi.

3991886

captcha