IQNA

Msahafu wa miaka 600 ulionadikwa kwa mkono Uturuki

17:46 - November 16, 2021
Habari ID: 3474565
TEHRAN (IQNA) Msahafu ulioandikwa zaidi ya miaka 600 iliyopita unaonyesha katika Maktaba ya Nyaraka ya Ziya Bey nchini Uturuki.

Mshahafu huo wa kale ambao umewashangaza wengi ulitunukiwa maktaba hiyo na raia wa Uturuki uliandikwa mwaka 1473 Miladia na mwanakaligrafia wa Kiislamu wakati huo Meliki El Esberi.

Msahafu huo uliandikw akwa kutumia mbinu ya kaligrafia ya Muhaqqaq badala ya ile ya Naskh ambayo ilikuwa inatumika kwa wingi wakati huo. Kwa sasa ni wataalamu tu wanaoweza kuuona msahafu huo kwa karibu huku wageni wanaotembelea maktaba hiyo wakipata idhini tu ya kuona nakala ya kidijitali.

Mkurugenzi wa Maktaba ya Nyaraka ya Ziya Bey,  Dahiye Karagülle, anasema msahafu huo umeandikwa kwa njia maridadi yenye kumvutia kila anayeutazama.

3476515/

Kishikizo: msahafu ، qurani ، uturuki
Jina:
Baruapepe:
* maoni:
captcha