Messaoud Redouane Dris amechukua hatua hiyo kuwauunga mkono watu wa Palestina na kuonyesha upinzani wake dhidi ya mauaji ya kimbari yanayofanywa na Israel huko katika Ukanda wa Gaza.
Idris alitakiwa kukabiliana na mwanajudo wa Kizayuni, Tohar Butbul, katika raundi ya kumi na sita, katika uzani wa kilo 73, lakini hakupunguza uzani wake ili asichuane na raia huyo wa utawala wa Kizayuni wa Israel unaoendelea kuua watoto wa Gaza.
Dris anakuwa mwanajudo wa pili kutoka Algeria ambaye amejiondoa katika michuano ya Olimpiki kwa kukataa kucheza na mshindani wa Israel.
Mwaka 2021, mwanajudo wa Algeria Fethi Nourine alijiondoa kwenye pambano dhidi ya Butbul kwenye Michezo ya Olimpiki ya Tokyo.
Nourine alisema wakati huo kwamba amechukua uamuzi huo kutokana na uungaji mkono wake wa kisiasa kwa mapambano ya ukombozi ya Palestina. Shirikisho la Kimataifa la Judo lilimpiga marufuku kushiriki katika mchezo huo kwa miaka 10.
Maelfu ya watu wamekuwa wakiandamana mjini Paris wakitaka Israel ipigwe marufuku kushiriki Michezo ya Olimpiki ya mwaka huu kutokana na mauaji ya kimbari yanayofanywa na utawala huo katika eneo la Ukanda wa gaza huko Palestina.
3489273