IQNA

Kongamano la Kimataifa la Arubaini lafanyika Karbala

20:33 - September 28, 2021
Habari ID: 3474354
TEHRAN (IQNA)- Kongamano la Kimataifa la ‘Arubaini, Umaanawi na Fadhila za Kiakhlaqi’ limefanyika katika mji wa Karbala.

Wasomi kutoka nchi mbali wameshiriki katika kongamano hilo ambalo limeandaliwa na Kamati ya Kiutamaduni na Kielimu ya Arubaini Iran.

Kati ya waliohutubu katika kongamano hilo ni mbunge wa zamani wa Iran Naser Soudani, Mohammad Hadi Homayoun  ambaye ni mkuu wa Kituo cha Masomo ya Kiislamu na Mawasiliano katika Chuo Kikuu cha Imam Sadiq AS mjini Tehran na Bi. Tahereh Sadeghi mhadhiri wa chuo kikuu.

Hujjatul Islam Hamid Ahmadi, mkuu wa na Kamati ya Kiutamaduni na Kielimu ya Arubaini Iran amesema kwa ujuma wameandaa makongamano sita wakati wa matembezi ya Arubaini ya Imam Hussein AS mwaka huu mjini Karbala ambapo washiriki wamejadili maudhui mbali mbai za ulimwengu wa Kiislamu.

Maadhimisho siku ya Arubaini (Arobaini au Arbaeen) hufanyika kila mwaka tarehe 20 Safar, kwa mujibu wa kalenda ya Hijria Qamaria, baada ya kupita siku Arubaini tangu tarehe 10 mwezi wa Muharram, kwa ajili ya kukumbuka siku aliyouawa shahidi mjukuu wa Mtume SAW, Imam Hussein AS na masahaba zake ambao walijitolea roho zao kwa ajili ya kuhuisha dini ya Mwenyezi Mungu katika jangwa la Karbala mwaka 61 Hijria Qamaria. Haram Takatifu ya Imam Hussein AS iko katika mji huo wa Karbala.

Int’l Congress on ‘Arbaeen, Spirituality, Moral Vitrues’ held in Karbala

Int’l Congress on ‘Arbaeen, Spirituality, Moral Vitrues’ held in Karbala

3475816

captcha