IQNA

Arbaeen ya Imam Hussein AS

Mpango wa Afya Wazinduliwa huko Karbala kwa ajili ya Arbaeen

22:15 - September 05, 2022
Habari ID: 3475739
TEHRAN (IQNA) – Idara ya afya ya mkoa wa Karbala nchini Iraq imezindua mpango maalum wa afya kwa ajili ya maombolezo ya Arbaeen ya Imam Hussein AS.

Sabah al-Mousawi, mkuu wa idara hiyo, alisema mpango huo unatekelezwa ndani ya mfumo wa kanuni za kukabiliana na magonjwa ya kuambukiza, shirika rasmi la habari la Iraq INA liliripoti.

Alisema timu 75 za madaktari na hospitali 8 zitashirikiana katika kutekeleza mpango huo huku timu 50 za afya zitatumwa kusimamia usambazaji wa maji ya kunywa na chakula kwa mahujaji.

Kwa mujibu wa afisa huyo, magari 85 ya kubebea wagonjwa pia yatawekwa katika maeneo tofauti ndani na karibu na mji mtakatifu wa Karbala.

Pia alibainisha kuwa vituo vya chanjo katika jimbo lote vinaendelea kutoa chanjo kwa raia na juhudi za kuongeza uelewa juu ya hitaji la kuzuia kuenea kwa COVID-19 pia zinaendelea. Mamilioni ya waumini wanatazamiwa kufika Karbala katika siku zijazo kwa ajili ya Arbaeen.

Maadhimisho ya Arbaeen (Arubaini) ni mojawapo ya mikusanyiko mikubwa ya kidini duniani.

Siku hii huadhimishwa  siku ya 40 baada ya kumbukumbu ya kuuawa shahidi mjukuu wa Mtume Muhammad (SAW), Imam Hussein (AS) tarehe 10 Muharram katika Siku ya Ashura.

Kila mwaka, wafanyaziara, hasa kutoka Iraq na Iran, husafiri njia ndefu kwa miguu hadi Karbala, ambako ndiko kunako haram takatifu la Imam Hussein (AS).

Siku ya Arbaeen mwaka huu inasadifiana na Septemba 17 mwaka huu.

Wafanyaziara, hasa kutoka Iraq na Iran, husafiri njia ndefu kwa miguu hadi mji mtakatifu.

 

4083184

Habari zinazohusiana
captcha