IQNA

Mufti wa Oman ataka Ummah wa Kiislamu uwatetee Waislamu wa India

20:12 - September 29, 2021
Habari ID: 3474358
TEHRAN (IQNA)- Mufti Mkuu wa Oman Sheikh Ahmed bin Hamad Al-Khalili ametoa wito kwa Ummah wa Kiislamu duniani kuungana na kuwatetea Waislamu wa India.

Katika ujumbe aliouandika katika ukurasa wake wa Twitter, Mufti wa Oman amebainisha masikitiko yake kuhusu hujuma na ukatili unaotendwa makundi yenye misimamo mikali dhidi ya Waislamu wa India. Makundi hayo ya kufurutu adha yanawahujumu Waislamu kwa himaya ya serikali ya India.

“Kwa jina la uanadamu, natoa wito kwa nchi zote zipendazo amani kuingilia na kusutisha hujuma hii na pia natoa wito kwa Ummah wa Kiislamu kuungana katika jambo hili.”

Kwa muda mrefu sasa chama tawala India cha BJP,chenye misimamo mikali ya Kihindu, kimekuwa kikitekeleza kampeni ya makusudi dhidi ya Waislamu wa eneo la Assam ambao ni zaidi ya asilimia 33 ya wakazi wa jimbo hilo la kaskazini mashariki.

Mwaka 2018, serikali ya Waziri Mkuu Narendra Modi iliwapokonya uraia mamilioni ya Waislamu wa Assam kwa madai kuwa ni wahajiri haramu kutoka nchi jirani ya Bangladesh.

Kuanzia Septemba 20 oparesheni ya kuwatimua Waislamu kutoka nyumba zao imeanza na hadi sasa familia 800 zimelazimishwa kuondoka.

4001201

captcha