Kwa Shahidi Soleimani, suala la Palestina lilikuwa mradi wa kuunganisha katika ngazi ya kitaifa na Umma wa Kiislamu, amesema Ahmed Abdulrahman katika mahojiano na Shirika la Habari za Qur'ani la Kimataifa (IQNA), katika kumbukumbu ya miaka 5 ya kuuawa kwa kamanda mkuu wa Iran.
Jenerali Soleimani, kamanda wa Kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu, na Abu Mahdi al-Muhandis, naibu mkuu wa Vikosi vya Hashdu Shabi vya Iran, pamoja na wanajihadi wenzao kadhaa, waliuawa katika shambulio la kigaidi la ndege isiyo na rubani la Marekani kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Baghdad mnamo Januari 3, 2020.
Abdulrahman aliiambia IQNA, “Tunafahamu jukumu muhimu la Haj Qassem Soleimani na Haj Abu Mahdi katika Palestina. Kwa kweli, mashahidi hawa wawili wakuu walikuwa na athari kubwa katika kuimarisha usalama katika eneo hilo, hasa wakati wa kuongezeka kwa magaidi wa kitakfiri wa Daesh (ISIS au ISIL) na makundi yao yanayohusiana, ambayo yalifanya vitendo vya uharibifu na mauaji katika nchi kadhaa, ikiwa ni pamoja na Iraq na Syria. Wao (wanachama wa Daesh) pia walifanya mashambulizi ya kigaidi katika nchi nyingine, ikiwa ni pamoja na Iran, Lebanon, na maeneo mengine mengi.”
Aliongeza, “Kwa maoni yangu, majukumu ya mashahidi hawa wawili yalikuwa ya msingi na ya kiutendaji katika kupambana na magaidi, na waliongeza morali au motisha ya vikosi vya muqawama. Mashahidi hawa wawili wakuu walifanya vitendo muhimu katika kipindi kifupi na kigumu sana, kwani mashambulizi ya kigaidi yalifanywa kwa msaada wa Marekani na madola mengine ya kikoloni katika. Mashahidi hawa wawili walifanikiwa kwa kiasi kikubwa katika kusimamisha na kuzuia mashambulizi haya katika maeneo mbalimbali, hasa Iraq, Syria, Lebanon, na Iran, na walikuwa na jukumu muhimu katika kuangamiza ugaidi.”
Alipoulizwa kuhusu athari za Mashahidi Soleimani na Al-Muhandis katika kubadilisha mlingano wa nguvu kwa manufaa ya harakati za Muqawama alisema, “Kwa kweli, mlingano wa nguvu ulionekana kubadilika wakati wa mashahidi hawa wawili mashuhuri. Katika nchi nyingi ndani ya mhimili wa muqawama, na hata zaidi ya hapo, kama vile Bosnia na mataifa mengine, tulishuhudia kwamba popote Waislamu walipokabiliana na changamoto, Haj Qassem Soleimani alikuwa akihudhuria kushughulikia masuala hayo.”
Alisema zaidi, “Al-Muhandis pia alitetea Iraq na Syria kutoka mstari wa mbele, akicheza jukumu muhimu katika nchi hizo. Inaweza kusemwa kweli kwamba haiba ya wanaume hawa wawili wakuu ilikuwa na athari kubwa kwa makamanda na vikosi vya upinzani, ambao walipata msukumo na morali kutoka kwao.”
“Tunajua kwamba mapambano yote ya vikosi vya muqawama huko Gaza katika mwaka uliopita yamekuwa matokeo ya vitendo vya Haj Qassem ndani ya Kikosi cha Quds, kilichoongozwa na maelekezo ya (Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu) Ayatullah (Seyed) Ali Khamenei.”
Abdulrahman aliendelea kusema kwamba “Haj Qassem aliona suala la Palestina kama suala kuu la ulimwengu wa Kiislamu, ambalo linapaswa kuungwa mkono kwa njia yoyote ile. Kwa Haj Qassem, suala la Palestina lilikuwa mradi wa umoja, kitaifa na Kiislamu, badala ya mradi wa kidini au kikanda tu – kama wengine wanavyotaka kuonyesha. Hii ndiyo sababu alikuwa na nafasi kubwa kati ya vikosi vyote vya mhimili wa muqawama, na historia itamkumbuka shahidi huyu mkuu kama kiongozi na kamanda ambaye alipanua mhimili wa upinzani.”
Akirejelea hasara iliyosababishwa na kuuawa kwa mashahidi hawa wawili wakuu, alisema, “Katika siku hizi, hasa katika hali maalum na mabadiliko makubwa tunayokabiliana nayo, tumempoteza Haj Qassem, al-Muhandis, na pia Sayed Hassan Nasrallah. Hata hivyo, tuna uhakika kwamba ndugu zao na wenzake wataendelea na njia hii.”
4257298