IQNA

Kongamano la umoja wa Kiislamu ni kwa maslahi ya Waislamu duniani

16:00 - October 21, 2021
Habari ID: 3474450
TEHRAN (IQNA)- Msomi mmpja wa Pakistan ameipongeza Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kwa kuandaa kila mwaka kongamano la kimataifa la umoja wa Kiislamu na kusema hatua hiyo ni huduma kubwa wa Waislamu duniani.

Akihutubu kwa njia ya intaneti katika Kongamano la 35 la Kimataifa la Umoja wa Kiislamu, Maulana Abdul Haq Hashmi ambaye ni mwenyekiti wa jumuiya ya Jamaat-e-Islami Balochistan ya Pakistan amesema kongamano hilo ni fursa ya kipekee ya  kuhimiza umoja na mshikamano miongoni mwa Waislamu.

Amekumbusha kuhusu jitihada za maulamaa wa Kisunni na Kisuia za kuleta umoja  na kuwataka waliongoza harakati hiyo kuwa ni pamoja na Sheikh Hassan al-Bana, Sheikh Mohammad Taqi Qomi, Sheikh Shaltut, na baada ya ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran, Imam Khomeini MA na mrithi wake, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Sayyid Ali Khamenei.

Hashmi pia amewaenzi wanazuoni wengine wa Iran waliobeba bendera ya umoja na kkurubisha madhehebu za Kiislamu hasa Ayatullah Vaezzadeh Khorasani and Ayatullah Mohammad Ali Taskhiri.

Mkutano wa 35 wa Kimataifa wa Umoja wa Kiislamu ulianza Jumanne hapa mjini Tehran kwa kaulimbiu ya "Umoja wa Kiislamu; Amani na Kuepukana na Mifarakano na Mizozo" kwa hotuba ya Rais Ebrahim Raisi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.

Mkutano huo wa siku tano, ambao kwa sababu ya kuchunga miiko na miongozo ya kiafya ya kujiepusha na janga la corona unafanyika kwa mahudhurio ya moja kwa moja na kwa njia ya intaneti, unahudhuriwa na washiriki kutoka Iran na nchi 39 duniani.

Inafaa kuashiria hapa kuwa, Tuko katika siku tukufu za kuadhimisha Maulid ya Mtume Mtukufu wa Uislamu Mohammad al Mustafa SAW, siku ambazo ni maarufu kama Maulidi. Waislamu wa madhehebu ya Sunni wanaadhimisha siku hiyo tarehe 12 Rabiul Awwal na Waislamu wa Madhehebu ya Shia wanamini siku hiyo ni tarehe 17 Rabiul Awwal.

Miaka mingi iliyopita, Hayati Imam Khomeini MA, Kiongozi mwanzilishi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran, ambaye binafsi alikuwa mstari wa mbele kulingania umoja wa Kiislamu alipendekeza kuwa, muda uliopo baina ya tarehe hizo mbili uwe ni "Wiki ya Umoja wa Waislamu" kwa lengo la kuimarisha mashikamano na udugu baina ya madhehebu za Kiislamu.

4006836

Jina:
Baruapepe:
* maoni:
captcha