IQNA

13:05 - January 19, 2022
Habari ID: 3474825
TEHRAN (IQNA)- Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesisitiza kuwa: Ushirikiano kati ya Iran na Russia unajenga amani na usalama na utazuia sera za kujichukulia maamuzi ya upande mmoja katika kanda hii.

Sayyid Ebrahim Raisi amesema leo Jumatano katika uwanja wa ndege wa Mehrabad kabla ya kuondoka Tehran akilekea Moscow kwamba: Ziara hiyo inafanyika kwa mwaliko wa Rais Vladimir Putin wa Russia na kwamba juhudi zitafanyika ili kukuza udiplomasia wa kikanda.

Raisi ameongeza kuwa: "Uhusiano mzuri wa Iran na majirani zake wote hususan Russia katika masuala ya kisiasa, kiuchumi na kibiashara, unaweza kuleta mabadiliko makubwa katika uhusiano wetu na Russia."

Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema: Iran ni nchi huru, yenye nguvu na taathira katika eneo la Magharibi mwa Asia, na Russia ni nchi muhimu, yenye nguvu na taathira kubwa.

Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ameondoka mapema leo mjini Tehran akiongoza ujumbe wa ngazi ya juu.

kulu ya Rais wa Russia, Kremlin, ilitangaza jana kwamba akiwa mjini Moscow, Rais wa Iran atazungumza na Putin kuhusu utekelezaji wa mapatano ya nyuklia ya JCPOA.

Viongozi hao wawili pia watabadilishana mawazo kuhusu uhusiano wa pande mbili hasa kuhusu miradi ya pamoja ya kiuchumi na kibiashara.

Halikadhalika Rais wa Iran anatazamiwa kuhutubia kikao cha Bunge la Russia, Duma, na kisha atakutana na Wairani waishio Russia katika safari hiyo ya siku mbili.

4029685

Kishikizo: iran ، raisi ، russia ، putin
Jina:
Baruapepe:
* maoni:
* captcha: