IQNA

Wanafunzi Jordan wakataa msaada wa masomo wa UAE-Israel

11:31 - November 18, 2021
Habari ID: 3474573
TEHRAN (IQNA)- Wanafunzi nchini Jordan wamekataa msaada wa masomo wa chuo kikuu kimoja cha Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) baada ya kubainika kuwa msaada huo unatolewa kwa ushirikiano na utawala wa Kizayuni wa Israel.

Ujumbe wa Chuo Kikuu cha Akili za Kubuni (AI) Cha Mohammad Bin Zayed nchini UAE Jumanne ulifanya kikao na wanafunzo wa Chuo Kikuu cha Teknolojia ya Habari na Mawasiliano cha Jordan kujadili mpango huo.

Wakati wa kikao hicho wanafunzi waligundua kuwa, Taasisi ya Sayansi ya Weizmann ya utawala haramu wa Israel ni sehemu ya mpango huo na papo hapo wanafunzi wakaitisha maandamano kulaani uhusiano na utawala wa Israel unaokaliwa ardhi za Palestina kwa mabavu.

Maandamano yamefanyika pia katika vyuo vikuu vingine vya Jordan huku wanafunzi wakitilia shaka nia ya ujumbe huo wa UAE. Chuo Kikuu cha Hashemite kimefuta mkutano uliokuwa umepenga na maafisa wa UAE kufuatia kashfa hiyo.

Utawala wa Kizayuni wa Israel uko mbioni kutekeleza njama ya kuanzisha uhusiano nan chi za Kiarabu chini ya ule mpango wa 'Mapatano ya Abraham (Ibrahim)' ambayo yanaungwa mkono na Marekani. Hadi sasa UAE, Bahrain, Sudan na Morocco zimeanzisha uhusiano na Israel kwa msingi wa mpango huo ambao ni usaliti wa wazi kwa malengo matukufu ya ukombozi wa ardhi za Palestina zinazokoloniwa na Israel.

4014033

Kishikizo: jordan israel abraham uae
captcha