IQNA

Makundi ya Palestina yalaani safari ya waziri wa Israel huko Bahrain

13:01 - October 02, 2021
Habari ID: 3474372
TEHRAN (IQNA)- Harakati kadhaa za kupigania ukombozi wa Palestina zimelaani vikali hatua ya ufalme wa Bahrain kumpokea waziri wa mambo ya nje wa utawala haramu wa Israel.

Katika taarifa ya pamoja siku ya Ijumaa, harakati za ukombozi wa Palestina ambazo ni Hamas, Jihad Islami na Kamati za Mapambano, zimesema hatua ya kijuba ya baadhi ya nchi za Kiarabu na Kiislamu kuruhusu utawala wa Kizayuni wa Israel kufungua balozi katika nchi hizo ni kinyume cha matakwa ya wananchi ambao wanataka kuona Palestina inatkombolewa kutoka makucha ya utawala ghasibu wa Israel.

Taarifa hiyo imesema kufunguliwa ubalozi wa utawala bandia wa Israel katika mji mkuu wa Bahrain, Manama, ni usaliti kwa Uislamu, utambulisho wa Kiarabu na pia ni usaliti hasa kwa watu wa Palestina na Bahrain.

Ubaloz wa utawala bandia wa Israel mjini Manama ulifunguliwa Alhamisi katika hafla iliyohudhuriwa na waziri wa mambo ya nje wa utawala huo Yair Lapid akiwa ameandamana na mwenzake wa ufalme wa Bahrain Abdullatif al Zayani.

Wakati huo huo, Waziri wa Mashauri ya Kigeni ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, hatua ya utawala wa Bahrain ya kumkaribisha na kumpokea Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa utawala bandia wa Israel ni khiyana na usaliti wa wazi kwa malengo matukufu ya Wapalestina na muqawama wa Palestina na kubainisha kwamba, zawadi ya utawala wa Kizayuni kwa Bahrain na eneo ni machafuko tu.

Hussein Amir-Abdollahian ameandika katika ukurasa wake wa mtanado wa kijamii wa twitter: Hatua ya Bahrain ya kumpokea Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa utawala bandia wa Israel ni khiyana na usaliti wa wazi kwa malengo matukufu ya Wapalestina na muqawama wa Palestina.

Aidha amendika: Sisi hatutambui isipokuwa nchi moja tu, nayo ni Palestina, mji mkuu wake ni Quds, na bila shaka hakuna unacholeta utawala huo ghasibu  kwa Bahraina na eneo isipokuwa machafuko na ukosefu wa amani.

Kwingineko, wananchi wa Bahrain wameendelea kufanya maandamano makubwa katika miji mbalimbali ya nchi hiyo kulaani safari ya Waziri wa mashauri ya Kigeni ya utawala haramu wa Kizayuni wa Israel katika nchi yao na kuanzishwa uhusiano wa kawaida na Tel Aviv.

Mwezi Septemba mwaka jana (2020) na kwa upatanishi wa aliyekuwa Rais wa wakati huo wa Marekani Donald Trump, Bahrain ilisaini mkataba uliopewa jina la Makubaliano ya Abraham, wa kufanya mapatano na utawala ghasibu wa Israel na kuanzisha rasmi uhusiano wa kidiplomasia na Tel-Aviv. 

4001614

 

captcha