IQNA

Mwanamke Mwislamu polisi kuvaa Hijabu, Michigan, Marekani

0:41 - August 27, 2016
Habari ID: 3470537
Afisa Mwislamu wa kike katika polisi ya Marekani mjini Dearborn kwenye jimbo la Michigan amekuwa afisa wa kwanza eneo hilo kuhudumu akiwa amevaa sare ya Hijabu .

Televisheni ya Press TV imeripoti habari hiyo na kuongeza kuwa, wazazi yaani baba na mama wa afisa huyo wa polisi wana asili ya Lebanon.

Bi Amal Chammout amesema, ameamua kuwa mwanamke wa kwanza kuvaa Hijabu katika jeshi la polisi nchini Marekani ili kuwa kigezo kizuri kwa Wamarekani wote.

Wakati maafisa wa polisi katika majimbo mengine ya Marekani wakilalamikia kutengwa na kufanyiwa ubaguzi mkubwa, maafisa wa polisi wa Dearborn wamesisitiza kuwa, hatua ya Bi Amal ya kuvaa sare ya Hijabu itajenga uhusiano mzuri baina ya jamii ya Waislamu na jeshi hilo na pia wameamua kuruhusu jambo hilo ili kuonesha kuwa, wako watu wengi wenye mtazamo tofauti na wale wanaopinga vazi la Hijabu.

Kwa mujibu wa ripoti ya televisheni ya Press TV, Waislamu nchini Marekani wanakabiliwa na changamoto na vitisho vingi.

Mji wa Dearborn una idadi kubwa zaidi ya jamii ya Waislamu nchini Marekani.

/3525456


captcha