IQNA

Wairani wako tayari kutekeleza ibada ya Umrah masharti yakitimizwa

20:59 - January 19, 2022
Habari ID: 3474826
TEHRAN (IQNA)- Iran imetangaza kuwa tayari kuwatuma wananchi wake kuenda Saudi Arabia kutekeleza ibada ya Umrah iwapo masharti yatatimizwa.

Hayo yamedokezwa na Mkuu wa Shirika la Hija na Ziara za Kidini Iran Ali Ridha Rashidian ambaye amesema kufunguliwa ubalozi mdogo wa Iran katika Ufalme wa Saudi Arabia, kudhaaminiwa heshima na usalama wa Wairani ni kati ya masharti ambaye yamewekwa na Iran.

Amesema taasisi zote husika nchini Iran zimeshachukua hatua za kuanza mipango ya kuwatuma Wairani kuelekea Saudia kwa ajili ya Hija ndogo ya Umrah iwapo masharti hayo yatatimizwa.

Kuhusu Ibada ya Hija, Rashidian amesema Saudi Arabia bado haijatangaza maamuzi kuhusiana na nsuala hilo.

Mwaka 2019, raia 86,000 wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran walitekeleza ibada ya Hija na hivyo kuifanya nchi hii kuwa miongoni mwa nchi zilizo na idadi kubwa ya Mahujaji duniani.

4029708

Kishikizo: umrah iran rashidian saudi
captcha