IQNA

Sala ya Ijumaa katika Misikiti ya Makka na Madina yarejea hali ya kawaida

17:35 - October 23, 2021
Habari ID: 3474460
TEHRAN (IQNA)- Waislamu duniani kote wamepata furaha tele kuona Sala ya Ijumaa katika Misikiti Mitakatifu ya Makka na Madina imerejea katika hali ya kawaida huku waumini wakiwa wamejaa kikamilifu

Misikiti Mitakatifu ya Masjid al-Haram mjini Makka na Al-Masjid an-Nabawi mjini Madina ilifungwa Machi 2020 kutokana na janga la ugonjwa wa COVID-19. Hatua hiyo iliumiza nyoyo za waumini duniani kote hasa katika miji hiyo ya Makka na Madina.

"Ni Baraka kubwa kufika hapa msikitini na kuona umezungukwa na waumini, "amesema Abdullah Mahdi, mfanya kazi wa sekta binafsi na mkaazi wa muda mrefu wa Makka. "Bado lazima tuvae barakoa lakini hilo si muhimu kwani sasa kuna harakati na waumini wamejaa," ameongeza.

Jumamosi iliyopita Wizara ya Mambo ya Nje ya Saudi Arabia ilitangaza kuwa vizingti vya COVID-19 vinapunguzwa kote Saudi Arabia na kwamba Misikiti Mitakatifu ya Makka na Madina itaidhinishwa kuendelea na ibada kama kawaida bila kuwepo vizuizi vya idadi ya watu wanaoweza kusali hapo.

Pamoja na hayo hatua zimechukuliwa kuzingatia kanuniz za kiafya za kuzuia kuenea ugonjwa wa COVID-19. Wote wanaoshiriki katika Sala wanatakiwa kuvaa barakoa na wawe wamepata chanjo ya COVID-19.

Kila anayetakaa kufika katika misikiti hiyo mitakatifu kwa ajili ya Sala au Hija Ndogo ya Umrah anapaswa kujaza maelezo yake katika aplikesheni rasmi za simu za mkononi za  Eatmarna and Tawakkalna ili kupata idhini kabla ya kufika katika maeneo hayo matakatifu.

3476162/

Kishikizo: sala ya ijumaa ، Makka ، madina ، mitakatifu ، covid 19
Jina:
Baruapepe:
* maoni:
captcha