IQNA

Kikundi cha kwanza cha Wairani wanaoelekea Umrah chafika Madina

9:56 - August 23, 2025
Habari ID: 3481126
IQNA – Kikundi cha kwanza cha Wairano wanaotekeleza Umrah baada ya Hajj ya mwaka huu kimewasili Madina, Saudi Arabia baada ya kuondoka mapema Jumamosi asubuhi katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Imam Khomeini jijini Tehran.

Jumla ya wafanyaziyara 250 wameelekea  Saudi Arabia katika  misafara miwili. Sherehe ya kuwaaga imefanyika uwanjani na kuhudhuriwa na maafisa waandamizi wa Shirika la Hija na Ziyara la Iran.

Hujjatul Islam Seyed Hossein Roknoddini, Naibu wa Kitamaduni katika Ofisi ya Mwakilishi wa Kiongozi katika Shirika la Hija na Ziyara, almesema katika sherehe hiyo kwamba pamoja na mipango iliyopangwa vyema, mtaalamu wa dini ameteuliwa kwa kila kundi la Wairani wanaoshirki Umrah ambaye atakuwa na jukumu la kusimamia utekelezaji sahihi wa ibada na taratibu za Umrah.

Wakati wa msimu wa Umrah mwaka huu, kutakuwa na programu nyingi zitakazofanyika katika miji miwili ya Makkah na Madina, muhimu zaidi ikiwa ni vikao vya qiraa ya Qur’ani vitakavvyoongozwa maqari maarufu wa Qur’ani.

Hujjatul Islam Roknoddini amesisitiza kuwa lengo la kufanyika kwa programu hizi ni kuongeza ufahamu na maarifa kwa wanaoshiriki ibada ya Hija ndogo ya Umrah.

Alireza Bayat, Mkuu wa Shirika la Hija na Ziyara, alihutubia pia sherehe hiyo.

“Leo, ndege ya kwanza ya wanaotekeleza ibada ya Umrah inatoka Tehran. Mwezi huu, tumepanga safari mbili za kila siku kutoka Tehran na mkoa mwingine kuelekea Ardhi ya Wahyi kupitia viwanja 17 vya ndege, ” alisema.

Moja ya hatua zilizochukuliwa kurahisisha safari ya kuelekea Nyumba ya Allah "ni kwamba tumepunguza umbali wa usafiri ambapo safari kati ya miji miwili ya Makkah na Madina itafanywa kwa treni,” alieleza.

Umrah ni ibada ya Mustahabb (inapendekezwa lakini si ya lazima) kwa Waislamu ambayo wanaweza kuitekeleza wakati wowote wa mwaka, kinyume na ibada ya Hija ambayo ni ya lazima au ya faradhi kwa kila Muislamu aliye na uwezo wa kimwili na kifedha mara moja katika maisha yake na inaweza kutekelezwa tu katika siku za mwanzo za mwezi wa Kiislamu wa Dhul-Hijjah.

4301255

 
Kishikizo: umrah iran
captcha