Katika hafla hiyo iliyofanyika Jumanne katika Chuo Kikuu cha Tehran, iliyohudhuriwa na viongozi wa kidini na wasomi, akiwemo Hujjatul Islam Mostafa Rostami, Mkuu wa Ofisi ya Mwakilishi wa Kiongozi katika Vyuo Vikuu na Alireza Bayat, Mkuu wa Jumuiya ya Hijja na Hija, maafisa walisisitiza umuhimu wa kuwasaidia wanafunzi kutekelelza ibada ya Umrah.
Rostani amewashauri washiriki kujiandaa na ibada ya Umrah kwa kusoma kuhusu kanuni na umhuhimu wa ibada hii.
Bayat ameitaja Umrah kuwa ibada ya kiroho na kuongeza kuwa. "Kuwepo Umrah kwa akili changa kunaongeza hisia za kujitolea katika maeneo kama Makka na Madina," alisema.
Wanafunzi waliochaguliwa wataondoka nchini kupitia viwanja vya ndege vinne vilivyoteuliwa vyaTehran, Isfahan, Kerman, na Mashhad. Bayat amewataka wanafunzi kuzingatia kanuni nchini Saudi Arabia, kama vile vikwazo vya upigaji picha na matumizi ya mitandao ya kijamii.