IQNA

Hotuba ya Sayyid Hassan Nasrallah kwa mnasaba wa Mwezi wa Ramadhani

22:32 - March 30, 2022
Habari ID: 3475087
TEHRAN (IQNA)- Katibu Mkuu wa Harakati ya Hizbullah ya Lebanon anatazamiwa kutoa hotuba Ijumaa kwa mnasaba wa kuwadia Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.

Kwa mujibu wa taarifa, hotuba hiyo itarushwa mubashara au moja kwa moja kupitia televisheni ya Al Manar saa mbili na nusu usiku kwa wakati wa Beirut na Afrika Mashariki.

Sayyid Hassan Nasrallah atazungumza kuhusu masuala mbali mbali katika hotuba hiyo ambayo inasubiriwa kwa hamu na wengi.

4045661

captcha