IQNA

Kusimamishwa uanachama wa Russia Baraza la Haki za Binadamu UN ni ishara ya ubeberu wa Marekani

22:01 - April 08, 2022
Habari ID: 3475100
TEHRAN (IQNA)- Naibu mwakilishi wa kudumu wa Russia katika Umoja wa Mataifa anasema kuwa upigaji kura wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa kwa ajili ya kusimamisha uanachama wa Russia katika Baraza la Haki za Kibinadamu la Umoja wa Mataifa unaonyesha juhudi za Marekani kudumisha msimamo wake wa kibeberu.

Ni baada ya kuitishwa kikao cha tatu cha dharura cha Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa kuhusu vita vya Ukraine ambacho kimefanyika usiku wa kuamkia leo kwa ombi la Marekani na washirika wake kwa ajili ya kusimamisha uanachama wa Russia katika Baraza la Haki za Kibinadamu la UN.

Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa limesimamisha uanachama wa Russia katika Baraza la Haki za Kibinadamu la Umoja wa Mataifa kwa kura 93 za ndio, 24 zimepinga na nchi 58 zimejizuia kupiga kura.

Nchi 24 zikiwemo Algeria, Belarus, Cuba, Korea Kaskazini, Iran, Kazakhstan, Uchina, Russia, Syria, Uzbekistan, Tajikistan na Vietnam zilipiga kura kupinga kusimamishwa uanachama wa Russia katika Baraza la Haki za Binadamu la UN.

Naibu mwakilishi wa Russia katika Umoja wa Mataifa, Gennady Kuzmin, alisema Alhamisi ya jana katika kikao cha Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa kilichopiga kura ya kusimamisha uanachama wa Russia katika Baraza la Haki za Kibinadamu kwamba: "Kura hii ni jaribio la Marekani la kudumisha msimamo wake wa kibeberu."

Afisa huyo wa Russia ameelezea kwamba, kura ya Baraza Kuu ya kusitisha uanachama wa Russia katika Baraza la Haki za Kibinadamu ni jaribio la Merekani la kudumisha udhibiti kamili.

Baraza la Haki za Kibinadamu la Umoja wa Mataifa lenye makao yake makuu mjini Geneva, lilianzishwa mwaka 2006 na lina wajumbe 47 waliochaguliwa na Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa. Baraza hilo sasa litabakia na wajumbe 46 baada ya kusimamishwa uanachama wa Russia iliyopaswa kuwa mwanachama hadi 2023. 

4047248

captcha