Akizungumza alipotembelea msikiti wa Bordj Bou Arreridj kaskazini mwa nchi, Youssef Belmehdi amesisitiza kuhusu nafasi ya misikiti na vyuo vya Qur'ani katika kuimarisha utambulisho wa kitaifa Algeria.
Aidha amesema wizara yake imejenga misikiti na vituo vya Kiislamu kwa msaada wa wafadhili na kuongeza kuwa, serikali ya sasa ya Algeria ina azma ya kuutumikia Uislamu.
Belmehdi amesema kuanzisha shule za Qur'ani na kufunguliwa misikiti ni moja ya njia za kueneza fikra za misimamo ya wastani na amani na kuzuia misimamo mikali ya kidini.
Halikadhalika amesema wizara yake iko tayari kuukaribisha Mwezi Mtukufu wa Ramadhani na kuongeza kuwa shughuli zote za ibada misikiti zitafanyika kwa kuzingatia kanuni za kiafya zilizowekwa ili kuzuia kuenea ugonjwa wa COVID-19.