IQNA

Waislamu na michezo
17:06 - May 28, 2022
Habari ID: 3475305
TEHRAN (IQNA)- Mesut Ozil, mchezaji wa zamani wa timu ya taifa ya soka ya Ujerumani, alihudhuria sala ya Ijumaa katika Msikiti Mkuu wa Istiqlal katika mji mkuu wa Indonesia Jakarta.

Ozil alitembelea msikiti huo mkubwa, moja ya nembo za jiji hilo, chini ya makubaliano na Wizara ya Utalii ya Indonesia ili kuitangaza nchi hiyo.

" Assalamu Aleykum, Asante kwa kuwa nami hapa. Lengo langu daima lilikuwa ni kusali katika msikiti huu mzuri na nyinyi," Ozil aliwaambia waandishi habari baada ya sala.

Mchezaji huyo wa Ujerumani mwenye asili ya Uturuki alikabidhi jezi ya Timu ya Soka ya Fenerbahçe ya Uturuki kwa imamu mkuu wa msikiti huo, Sheikh Nasaruddin Umar.

Kiungo huyo mwenye umri wa miaka 33 alifanya mkutano na waandishi wa habari pamoja na Waziri wa Utalii na Uchumi wa Ubunifu wa nchi hiyo Sandiaga Uno kabla ya kufika msikitini.

Kisha Ozil alitembelea kiwanda ambacho bidhaa zenye nembo ya huzalishwa na kukutana na maafisa wa Klabu ya Bali United kabla ya kuhudhuria mafunzo yaliyoandaliwa kwa ajili ya vijana kwenye Uwanja wa Gelora Bung Karno.

Wakati wa uchezaji wake, Ozil alichezea klabu zenye majina makubwa ikiwa ni pamoja na Real Madrid na Arsenal, akibeba Vikombe vinne vya FA vya Uingereza mnamo 2014, 2015, 2017 na 2020 na kushinda taji la La Liga la Uhispania 2012 akiwa na Real Madrid.

Alijiunga na Fenerbahce kwa uhamisho wa bila malipo kutoka Arsenal Januari 2021 na kufunga mabao tisa katika mechi 37 za klabu hiyo ya Istanbul.

Hata hivyo, Ozil aliondolewa kwenye kikosi cha Fenerbahce bila maelezo mwezi Machi.

Alifunga mabao 23 katika mechi 92 alizoichezea Ujerumani.

3479077

Kishikizo: ozil ، ujerumani ، soka ، indonesia
Jina:
Baruapepe:
* maoni:
* captcha: