IQNA

Mwokozi

Mtafiti wa Kijapani: Umahdi ni ufunguo wa kuuelewa Uislamu

7:19 - August 12, 2024
Habari ID: 3479266
IQNA – Itikadi ya Umahdi ni ufunguo wa kuelewa Uislamu na utamaduni wake, amesema mtafiti wa Kijapani.

Ninaamini kwamba Umahdi ni itikadi muhimu katikak kuuelewa Uislamu na utamaduni wake. Kwa wasio Waislamu kufahamu kwa hakika falsafa na utamaduni wa Kiislamu, lazima kwanza waelewe maana ya Umahdi,” Dk. Ryo Mizukami, mtafiti kutoka Taasisi ya Utafiti wa Lugha na Tamaduni za Asia na Afrika katika Chuo Kikuu cha Tokyo cha Mafunzo ya Kigeni, amesema katika mazungumzo na Shirika la Habari za Qur'ani la Kimataifa (IQNA).

Ulimwengu umejaa vita, ukandamizaji, na changamoto nyinginezo ambazo mara nyingi watu hawawezi kutatua peke yao, alisema, na kuongeza, "Kwa maoni yangu, daima kuna matumaini kwa mtu kuingilia kati na kutatua matatizo haya na ukosefu wa haki."

Mizukami amesema kuwa juhudi zaidi zinahitajika ili kutambulisha Umahdi kwa wasiokuwa Waislamu, akiongeza kuwa kutambulisha Msikiti wa Jamkaran ulioko mkoani Qom, Iran kunaweza kuwa mbinu madhubuti kwa ajili hiyo.

Alipoulizwa kuhusu chanzo cha kuvutiwa kwake na historia ya Uislamu, alisema, “Kwa utafiti wangu wa shahada ya kwanza, nilichagua kuzingatia historia ya Uislamu. Wakati huo, nilihisi kwamba watu wengi wa Japani hawakuthamini kikamilifu mtazamo anuai ndani ya utamaduni wa Kiislamu. Hilo lilichochea shauku yangu ya kuchunguza mada hiyo nikiwa Mjapani. Nilikuwa na shauku ya kuelewa mitazamo mbalimbali ndani ya historia na utamaduni wa Kiislamu.”

Akiashiria makala aliyoiandika kwa lugha ya Kijapani kuhusu mitazamo ya Ahul Sunna kuhusu Umahdi mwaka jana, mtafiti huyo alisema, “Nimeona inavutia kwamba baadhi ya wanachuoni wa Kisunni wameonyesha heshima kwa Maimamu kumi na wawili wa madhehebu ya Shia na wameandika kuhusu fadhila zao. Ilikuwa nukta ya kuvutia sana kujua kwamba baadhi ya wasomi wa madhehebu za Ahul Sunna wametoa maelezo ya kina kuhusu Umahd.”

"Kwa maoni yangu, hili ni muhimu kwa mahusiano ya Shia naSunni," alisema na kuongeza, "Kumekuwa na mabadilishano ya hadithi na mafundisho kati ya wanachuoni wa Shia na Sunni juu ya mada hii, ambayo ni muhimu kwa kuelewa Uislamu na Umahdi."

 "Katika masomo yangu kuhusu historia ya Uislamu, hasa kuhusu heshima kwa Ahlul-Bayt (AS) na Maimamu kumi na wawili wa Shia, nimeona jinsi walivyoheshimiwa sio tu na Waislamu wa madhehebu ya Shia bali pia na Waislamu wa madhehebu ya Sunni," alisema. .

Hadith inayojulikana sana katika vyanzo vya Waislamu inawafananisha Ahlul-Bayt na nyota za angani, zikiwaongoza Waislamu na kuwa viongozi wao. Hadith hii inaangazia heshima na umuhimu mkubwa ambao Waislamu, Shia na Sunni, wanao kwa Ahlul-Bayt (AS), aliongeza mwanazuoni huyo wa Kijapani.

Alipoulizwa kuhusu marejeo yake ya Qur'ani Tukufu wakati wa utafiti wake, Mizukami alisema, “Masomo yangu ni zaidi ya Uislamu kwa ujumla. Pia ninazama katika kazi za wanazuoni wa Kiislamu wa Shia na Sunni. Lengo kuu la utafiti wangu ni jinsi wasomi hawa wanavyoitumia Qur'ani Tukufu kuunga mkono maoni yao. Wakati wowote ninapokutana na nukuu kutoka kwa Qur'ani, ninahakikisha kwamba ninarejelea maandishi moja kwa moja na kuzingatia dhamira ya matumizi yake. Vile vile, ninaiingiza Qur'ani  katika utafiti wangu, nikitegemea sana tafsiri mbalimbali.”

Tafsiri ni "muhimu," alisisitiza, akiongeza kwamba kwa kulinganisha tafsiri na tarjuma za Kijapani na Kiingereza, amepata "ufahamu wa kina" wa Qur'ani.

Watafiti hao walisema anavutiwa zaidi na uhusiano kati ya wanazuoni wa Shia na Sunni linapokuja suala la kuandika kuhusu fadhila za Maimamu.

Wajapani wengi na Wamagharibi wanaamini kimakosa kwamba Maimamu wa Shia ni muhimu tu kwa Shia; hata hivyo, Ahlul-Bayt (AS) wana umuhimu mkubwa kwa Waislamu wote,” alisisitiza.

"Kwa bahati mbaya, wasiokuwa Waislamu mara nyingi hudhani kwamba Sunni na Shia daima wako kwenye migogoro, lakini historia ya Uislamu inaonyesha kwamba uhusiano wao umekuwa muhimu na wa ushirikiano," Mizukami aliongeza.

Inafaa kuashirikia hapa kuwa Imam Mahdi (Mwenyezi Mungu Aharakishe kudhihiri Kwake) ni Imamu wa 12 wa madhehebu ya Shia Ithnaashari na alizaliwa huko katika mji wa Samarra, Iraq ya leo, tarehe 15 Shaaban 255 Hijiria. Imam Mahdi (af) alichukua jukumu la ukhalifa wa kuongoza Umma wa Kiislamu mwaka 260 Hijiria kufuatia kuuawa shahidi baba yake mpendwa Imam Hassan Askary (AS). Alichaguliwa kuhudumia nafasi hiyo muhimu na Mwenyezi Mungu mwenyewe, uongozi ambao bado unaendelea hadi leo hata baada ya kupita miaka zaidi ya elfu. Imam Mahdi (AS) ambaye hivi sasa yuko kwenye ghaiba yaani haonekani machoni pa walimwengu kwa amri ya Mwenyezi Mungu, atadhihiri tena na kuubadilisha kabisa ulimwengu kiuongozi na hivyo ndiye mwokozi anayesubiriwa.

Kudhihiri kwa Imam huyo wa mwisho, kunahitajia kupita wakati na kukomaa kwa akili, elimu na akhlaqi (maadili) ya watu na kuwa kwao tayari kwa ajili ya kushirikiana naye wakati muwafaka. Imam huyo wa mwisho wa Mwenyezi Mungu atawaongoza wanadamu wote kwenye njia nyoofu kuelekea kwa Muumba wao wakati ambao atapata fursa ya kuunda serikali itakayosimama juu ya misingi ya mafundisho ya Mwenyezi Mungu, kutekeleza uadilifu na kuheshimu sheria, na bila shaka jambo hilo litawezekana tu wakati wanadamu watakapokuwa tayari kukubali na kufuata miongozo ya mbinguni.

3489452

Kishikizo: imam mahdi
captcha