IQNA

Ahul Bayt AS

Waislamu wa madhehebu ya Shia Tanzania washerehekea Idi ya Nisf-Shaaban

20:27 - February 20, 2024
Habari ID: 3478382
IQNA – Waislamu wa madhehebu ya Shia nchini Tanzania wameanza kusherehekea Idi ya Nisf-Shaaban, kuadhimisha kumbukumbu ya kuzaliwa kwa Imam Mahdi (Mwenyezi Mungu aharakishe kudhiri kwake).

Vituo mbalimbali vya Waislamu wa madhehebu ya Shia katika nchi hiyo ya Kiafrika husherehekea hafla hiyo adhimu kila mwaka.

Sherehe hizo ni pamoja na hotuba za kidini na qasida, kwa mujibu wa Kituo cha Utamaduni cha Iran nchini Tanzania.

Wazungumzaji mashuhuri kutoka nchi zingine, haswa nchi zinazozungumza Kiingereza, wanaalikwa kutoa hotuba kwenye programu.

Sherehe moja kama hiyo ilifanyika katika Kituo cha Kiislamu cha Al-Mahdi katika mji mkuu wa Dar es Salaam.

Sherehe hiyo ilihudhuriwa na balozi wa Iran na mwambata wa kitamaduni, mwakilishi wa Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Al-Mustafa na idadi ya Wairani wanaoishi Tanzania.

Mwaka huu, siku ya 15 ya mwezi wa Hijri wa Shaaban, unaojulikana kama Nisf Shaaba, itakuwa Jumapili, Februari 25.

3487260

Kishikizo: imam mahdi 15 Shaaban
captcha