IQNA

Ibada ya Hija

Saudia yatakiwa iache kutumia Hija kama eneo la kukandamiza wapinzani

19:27 - June 17, 2022
Habari ID: 3475387
TEHRAN (IQNA)- Mashirika ya kimataifa ya kutetea haki za binadamu yameishutumu Saudi Arabia kwa kuingiza siasa katika ibada ya Hija na kuwakandamiza wapinzani.

Mashirika kadhaa ya kutetea haki za binadamu na mashirika ya Kiislamu yamejiunga na kampeni ya kulaani utawala wa kifalme Saudia kwa madai ya kutumia ibada ya Hija kama njia ya ukandamizaji, ama kwa kuwazuia baadhi ya Waislamu kuhudhuria Hija au kuwahadaa wengine waingie  nchini humo, lakini wakamatwe na kupelekwa katika nchi ambako wako hatarini.

Taasisi Sanad Rights Foundation ilisema katika taarifa yake siku ya Alhamisi kwamba mamlaka za Saudia zinatumia ibada ya Hija na Umrah kama njia ya "kuwakandamiza wapinzani" wanaopinga sera za nchi hiyo.

"Serikali ya Saudia mara kwa mara inaingiza siasa kwenye Misikiti Miwili Mitukufu ya Makka na Madina, na kuifanya Hijja na Umra kuwa chombo cha ukandamizaji, njia ya kuwaondoa wapinzani, na njia ya kuunga mkono baadhi ya tawala za kidikteta," ilisema taarifa ya taasisi hiyo..

Mnamo mwaka wa 2019, kulikuwa na Waislamu milioni 2.5 ulimwenguni kote walishiriki ibada ya Hajj. Walakini, ni Wasaudi 1,000 pekee waliofanya ibada ya kila mwaka ya Kiislamu mnamo 2020 katika kilele cha janga la Covid-19. Idadi hiyo iliongezeka hadi mahujaji 60,000 wa Saudi mnamo 2021.

Mwaka huu, Wizara ya Hija na Umra ya ufalme huo ilitangaza kuwa idadi ya mahujaji imefikia milioni moja. Mahujaji wote lazima wawe na umri wa chini ya miaka 65, wawe wamechanjwa kikamilifu dhidi ya Covid-19, na waonyeshe kipimo cha antijeni hasi ndani ya saa 72 baada ya kufika Saudi Arabia.

Wakati ibada ya Hija imefunguliwa kwa Waislamu kote ulimwenguni, mashirika ya kutetea haki za binadamu yana wasiwasi juu ya ulinzi na usalama wa Mahujaji wanaohudhuria.

3479336

Kishikizo: Hija ، waislamu ، saudia ، shirika la habari
Jina:
Baruapepe:
* maoni:
* :