IQNA

Wahifadhi Qur'ani wahitimu katika Shule ya Kiislamu ya Kaduna nchini Nigeria

15:10 - August 29, 2022
Habari ID: 3475699
TEHRAN (IQNA) - Zaidi ya wanafunzi 80 waliohifadhi Qur'ani Tukufu kikamilifu na wamehitimu kutoka shule ya Kiislamu huko Kaduna, kaskazini mwa Nigeria.

Wanafunzi hao wamehitimu katika  Shule ya Abubakar Saddiq Li’tahfiz Wa Kirasatul Islamiyya katika hafla ya Jumapili.

Shirika la Habari la Nigeria (NAN) liliripoti kuwa wahitimu hao walikuwa 63 kutoka kitengo cha Kiislamu cha masomo ya msingi ya shule hiyo huku wakitoka darasa  maaalumu za kuhifadhi Qur'ani.

Mwalimu Mkuu wa Kitengo cha Kiislamu wa shule hiyo, Malam Ahmad Abubakar, alisema mahafali ya 14 ya sehemu ya msingi katika historia ya shule hiyo, ni hatua muhimu katika historia yake.

Alisema shule hiyo iliyoanzishwa mwaka 2000 ilianza masomo ikiwa na wanafunzi 13.

"Sasa tuna wanafunzi wengi katika sehemu mbalimbali za shule kwa sababu ya nidhamu na kuendelea kuwajengea wanafunzi wetu maarifa na tabia," alisema.

Abubakar alisema shule hiyo sasa ina sehemu za elimu ya Kiislamu na Magharibi, inayojumuisha sehemu ya kuhifadhi Qur'ani, sehemu ya elimu ya sekondari ya vijana na elimu ya Kiislamu.

Alisisitiza umuhimu wa elimu ya Kiislamu, akisema ni elimu ambayo itaongoza mwenendo wa mtu kupata mafanikio huko akhera.

Alitoa wito kwa wahitimu hao kuendelea kusoma hata baada ya kuhitimu huku akibainisha kuwa kujifunza hakuisha.

Vile vile ametoa wito kwa wazazi kutilia maanani sana elimu ya Kiislamu ya watoto wao, na kubainisha kuwa ndio ufunguo pekee wa kumfikia muumba wake kwa kutimiza maamrisho yake kwa maadili ya matendo mema.

3480262

captcha