IQNA

Mashindano ya Qur'ani

Mashindano ya Qur'ani Tukufu yazinduliwa katikati mwa Nigeria

21:20 - September 20, 2022
Habari ID: 3475814
TEHRAN (IQNA) – Toleo la 36 la mashindano ya kila mwaka ya Qur’ani lilizinduliwa katika sherehe katika mji wa Jos katikati mwa Nigeria.

Shindano hilo hufanyika kila mwaka katika eneo la serikali ya mitaa ya Jos Kaskazini katika jimbo la Plateau.

Akihutubia sherehe za ufunguzi, mwanachama mteule wa Jimbo la Bassa/Jos-Kaskazini la Shirikisho la Nigeria Muhammad Adam Alkali alitoa wito kwa wanasiasa kuachana na siasa chafu na chuki kwa manufaa ya Wanigeria.

"Lazima tuwe na umoja wa kusudi. Kunapaswa kuwa na msamaha na uvumilivu kati yetu," alisema.

Alkali, ambaye hivi karibuni alitangazwa mshindi wa uchaguzi mdogo wa Jimbo la Bassa/Jos-Kaskazini la Shirikisho la Nigeria, alisema uongozi ni wa Mwenyezi Mungu na humpa amtakaye wakati wowote.

"Lazima tuepuke uovu na kutuhumiana kwa sababu ya tofauti za kisiasa. Siasa ni maslahi tu. Leo, ninaweza kuwa katika chama cha PRP na mtu katika APC; kesho tunaweza kuwa pamoja katika chama kimoja cha siasa kwa sababu ya maslahi.

"Ndio, lazima kuwe na tofauti, lakini haipaswi kusababisha chuki ambayo itaweka maisha ya watu wetu hatarini," alisema.

Amesema Qur'ani tukufu imeweka msingi madhubuti, kwa mifano mingi ya jinsi binadamu anavyopaswa kuendesha maisha yake.

Mgeni rasmi Sheikh Mukhtar Adam, alisema siasa ni sehemu ya mfumo wa maisha ya Waislamu na inapaswa kutekelezwa kwa mujibu wa mafundisho ya Quran.

"Quran ni njia kamili ya maisha kwa kila Muislamu. Ni mwongozo kamili na kwa hivyo wanasiasa wetu wanapaswa kuzingatia ukweli kwamba wataulizwa kuwajibika kwa matendo yao, "alisema.

/3480556

captcha