IQNA

Waislamu wa Marekani

Kituo cha Kiislamu cha Naperville, Marekani chakamilisha awamu ya mradi wa msikiti

20:28 - December 21, 2024
Habari ID: 3479929
IQNA – Kituo cha Kiislamu cha Naperville (ICN) nchini Marekani kimekamilisha awamu ya awali ya mradi wake mpya wa msikiti wa futi za mraba 28,400 kwenye barabara ya 248th Avenue.

Msikiti huo umeanza shughuli zake Desemab 15, Rais wa Kituo cha Kiislamu cha Naperville Anees Rahman alithibitisha. Kituo hicho kilifanya ufunguzi wa faragha kwa wanajamii wake, huku kukiwa na mipango ya hafla pana katikati ya Januari, Chicago Tribune iliripoti Ijumaa.

Rahman alibainisha kuwa mjumuiko ujao utakaribisha wakazi wa eneo hilo, vyama vya wamiliki wa nyumba, watoa huduma wa kwanza, maafisa wa jiji, na washikadau wengine katika jamii.

Rahman alionyesha kufurahishwa na maendeleo ya mradi huo, akisema, "Kila mtu amefurahiya sana. Nimefurahiya sana. Unajua, kama rais wa ICN, sijachukua likizo kwa miaka kadhaa. Kwa hivyo ninaenda likizo, sasa [msikiti] umefunguliwa rasmi.”

Ujenzi wa msikiti huo ulianza mnamo Septemba 2022.

Msikiti unawakilisha hatua ya kwanza tu katika mpango wa maendeleo wa muda mrefu wa kituo hicho cha Waislamu ambacho kina ukubwa wa  ekari 13.3 kusini magharibi mwa Naperville.

Awamu za siku zijazo za ujenzi zinalenga kujumuisha shule, ukumbi wa kijamii, ukumbi wa mazoezi, na upanuzi wa ziada wa msikiti.

Rahman alieleza kuwa awamu zinazofuata zinaweza kuchukua muda wowote kuanzia miaka mitano hadi kumi huku akibaini kuwa  kwa kiasi kikubwa kutegemeana na hali ya kifedha.

3491128

captcha