IQNA

Jinai za Israel

Waindonesia walaani walowezi wa Israel wanaovamia Misikiti ya Al-Aqsa, Ibrahimi

19:36 - September 29, 2022
Habari ID: 3475855
TEHRAN (IQNA) – Harakati ya Al-Aqsa ya Indonesia iimelaani vikalia hatua ya hivi karibuni ya walowezi wa Kizayuni wa Israel kusherehekea mwaka mpya wa Kiyahudi katika Msikiti wa Al-Aqsa huko al-Quds (Jerusalem) na Msikiti wa Ibrahimi huko Al-Khalil (Hebron).

Shughuli zilizofanywa kati ya Septemba 25-27 zilisababisha machafuko makubwa katika Ukingo wa Magharibi unaokaliwa kwa mabavu na utawala wa Kizayuni wa Israel.

Taarifa hiyo ilisema sherehe na matambiko hayo yanajumuisha unyanyasaji wa makusudi, kufuru na ugaidi dhidi ya utakatifu wa misikiti.

Kundi hilo lilionya kwamba vikiachwa bila kudhibitiwa, "vitendo hivi vya uchochezi" vinaweza kuzua mzozo wa kidini.

Taasisi hiyo ya Indonesia imeongeza kuwa kusherehekea mwaka mpya wa Kiyahudi katika misikiti hiyo ni ishara "kwamba Wazayuni hawana nia njema kabisa katika kujenga amani katika eneo na dunia."

Kundi hilo limewataka Waislamu kila mahali kujibu hujuma hiyo ya Wazayuni kwa hatua madhubuti.

"Kudumisha misikiti miwili mitukufu ni jukumu la Waislamu wote, sio Waislamu tu wa Palestina," ilisema taarifa hiyo.

3480670

Jina:
Baruapepe:
* maoni:
captcha