IQNA

Waislamu Marekani

Gwaride la Kila Mwaka la Waislamu lafanyika New York

14:03 - September 26, 2022
Habari ID: 3475844
TEHRAN (IQNA) – Gwaride la 38 la Kila Mwaka la Siku ya Umoja Waislamu wa Marekani lilifanyika Manhattan, jijini New York.

Idadi kubwa ya Waislamu  pamoja na maafisa wa Idara ya Polisi ya New York (NYPD) walishiriki katika gwaride hilo siku ya Jumapili.

Gwaride hili lilianza mtaa wa Madison Avenue kati ya East 24th na East 26th Street huko Manhattan, na kuwashirikisha Waislamu kutoka mataifa mengi ambao wanaishi Marekani.

Wanachama wa NYPD na Jumuiya ya Maafisa wa Kiislamu pia waliandamana.

Waandamanaji walisikika wakitoa nara za takbir, Allahu Akbar. Gwaride hilo pia lilihusisha malori ya kubeba mifano ya Kaaba na  Qubbat aṣ-Ṣakhra ambalo liko kiwanja cha Msikiti wa al-Aqsa huko al-Quds.

Washiriki wa gwaride hili pia walisali Sala ya Jamaa na waliandaa tamasha la chakula na na halikadhalika maonyesho ya kitamaduni.

3480630

Kishikizo: new york ، waislamu ، marekani
Jina:
Baruapepe:
* maoni:
captcha