Wakili Rafik Chekkat, mwanzilishi wa jukwaa la kukabiliana na chuki dhidi ya Uislamu, aliripoti kwamba Maarifi aliwekwa chini ya ulinzi wa nyumbani kwake siku ya Alhamisi.
Alikosoa kukamatwa kwake, akisisitiza kwamba muuguzi huyo anakandamizwa wakati wanajeshi wa Ufaransa waliopigana huko Gaza "wanatembea huru bila kujali."
Thomas Portes, mbunge kutoka chama cha La France Insoumise (LFI), alithibitisha kuachiliwa kwa Maarifi kutoka kizuizini.
Alitoa maoni yake kwenye mtandao wa kijamii wa X, akisema, "Msako wa nyumba mbele ya wanafamilia ni ishara isiyo na shaka kuwa lengo lilikuwa kutisha sauti zinazopazwa kuunga mkono watu wa Palestina na kutaka kusitishwa kwa mapigano mara moja."
Maarifi alikuwa ameshiriki katika mikutano ya watetezi wa haki za Palestina nchini Ufaransa, akielezea uzoefu wake kuhusu hali mbaya ya Gaza. Ametoa wito wa kusitishwa kwa mapigano mara moja huko Gaza na akapendekeza kususia makampuni yanayounga mkono utawala wa Israel.
Wakati alipokuwa Gaza, Maarifi alijitolea kama daktari katika hospitali ya Ulaya huko Khan Yunis.
Utawala wa Israel ulianzisha vita vyake vya kutisha dhidi ya Gaza tarehe 7 Oktoba mwaka jana baada ya makundi ya muqawama wa Palestina kutekeleza Operesheni ya Kimbunga cha Al-Aqsa ili kukabiliana na ongezeko la ukatili dhidi ya Wapalestina.
Utawala katili wa Israel hadi sasa umeua Wapalestina zaidi ya 40,900,na kuwaacha wengine zaidi ya 94,000 kujeruhiwa. Wengi wa waathiriwa ni wanawake na watoto.
Uchokozi huo wa kikatili umesababisha takriban wakazi wote wa Gaza kupoteza makazi huku pia ukiharibu hospitali nyingi na miundombinu mingine muhimu.
3489787