Maafisa wa haram hiyo tukufu wamesema kuwa alama za maombolezo ni ishara ya kuanza maandalizi ya mapokezi ya maelfu ya mahujaji wanaotarajiwa kufika kwa ajili ya tukio hili la kila mwaka.
Ahmad al-Zurkani, mkuu wa kitengo cha khuddam au wanaojitolea kuhudumu katika haram, amesema takriban wahudumu wa kujitolea wapatao 2,500 wataimarisha idara za huduma wakati wa maombolezo ya siku mbili.
“Watahusishwa na idara za huduma za kijamii, udumishaji wa utulivu, mambo ya wanawake, huduma za wageni, na pia kitengo cha kuongoza waliopotea,” alinukuliwa akisema kupitia tovuti ya haram.
Ameongeza kuwa kituo cha afya chenye jina la Mtume (SAW) pia kitaungwa mkono na wahudumu waliopata mafunzo, huku wakalimani na wataalamu maalum wakiwa tayari kuwahudumia wageni wa kimataifa.
“Wafanyakazi wa kujitolea wamesajiliwa katika kanzidata mahsusi, na vifaa vyote muhimu vimeandaliwa ili kuhakikisha wanaweza kutekeleza majukumu yao,” al-Zurkani alibainisha.
Mamlaka ya haram imeweka mpango wa kina wa kukidhi mahitaji ya mahujaji watakaokuja kutoa heshima kwa Imam Ali (AS) na kuomboleza wafat wa Mtume Muhammad (SAW), uliotokea Madina mwaka 11 Hijria (632 BK).
Tarehe 28 ya mwezi wa Hijria wa Safar, ambayo mwaka huu inatazamiwa kuwa Ijumaa, tarehe 22 Agosti, inaashiria kumbukumbu ya kufariki kwa Mtume Mtukufu (SAW) na pia kumbukumbu ya shahada ya Imam Hasan al-Mujtaba (AS).
3494328