IQNA

Shakhsia katika Qur'ani / 11

Juhudi za Miaka 120 za Nabii Saleh za Kuwaongoza Makafiri

17:05 - October 15, 2022
Habari ID: 3475935
TEHRAN (IQNA) – Nabii Saleh, Amani ya Mwenyezi Mungu Iwe Juu Yake –AS- alichaguliwa na Mwenyezi Mungu kuwa Mtume alipokuwa na umri wa miaka 16 na kwa miaka 120, alijaribu kuwaalika watu kwenye njia iliyonyooka lakini ni watu wachache waliokubali mwaliko wake na waliokolewa na adhabu ya Mwenyezi Mungu.

Saleh alikuwa nabii wa Kiarabu na aliyetoka katika kizazi au dhuria wa Nabii Nuh. Qur'ani inaashiria jina lake baada ya Nuh na Hud. Kulingana na vitabu vya historia, kumekuwa na pengo la miaka 100 kati ya Saleh na mtangulizi wake, Hud. Saleh ametajwa kuwa nabii wa tatu aliyewaalika watu kwenye Tauhidi.

Qur'ani Tukufu inarejelea jina la Saleh mara tisa katika Sura tofauti, lakini hajatajwa katika vitabu vya dini zingine.

Alipewa jukumu la utume akiwa na umri wa miaka 16, akichukua jukumu hilo kwa miaka 120. Alikuwa nabii wa kabila la Thamud katika bara Arabu. Kabila hili lilikuwa likiabudu masanamu 70 na Mwenyezi Mungu akamtuma Saleh kuwaongoza kutoka kwenye giza.

Kwa miaka mingi, Saleh alifanya kila juhudi kukuza imani ya Mwenyezi Mungu mmoja katika kabila lake lakini bila mafanikio. Hatimaye, anapendekeza changamoto katika majadiliano na jumuiya. Kwanza anauliza sanamu majina yao lakini hapati jibu. Kisha aliwataka watu waombe kitu kutoka kwa Mwenyezi Mungu.

Kisha watu wakamtaka Saleh amwambie Mungu wake aibue ngamia kutoka kwenye mawe na kwa mapenzi ya Mwenyezi Mungu, ngamia jike mwekundu alitoka milimani.

Kisha Saleh akalitaka kabila lake kumheshimu ngamia lakini watu wachache wakaamua kumwangamiza mnyama huyo. Kukanusha kwao haki ndio sababu ya Mwenyezi Mungu kuweka adhabu ya Mwenyezi Mungu juu ya Thamud.

Saleh na kundi la wafuasi wake walihamia maeneo kama vile Makka, Samarra, na Gaza. Kuna maeneo kadhaa huko Palestina leo ambayo yana jina la Saleh ambayo wanahistoria wanaamini yanaonyesha vizazi vya kabila la Thamud waliishi katika ardhi hizi. Kwa mujibu wa baadhi ya riwaya, Saleh alifariki dunia akiwa na umri wa miaka 280 na alizikwa katika makaburi ya Najaf ya Wadi Al-Salam katika Iraq ya leo.

captcha