IQNA

Shakhsia katika Qur’ani / 12

Nimrud; Mfalme ambaye aliangamizwa na mbu

21:46 - October 14, 2022
Habari ID: 3475929
TEHRAN (IQNA) – Nimrud amegeuka kuwa alama katika historia, alama ya mtu aliyejiona kuwa bwana wa ardhi na mbingu lakini akauawa na mbu.

Nimrud alikuwa mfalme wakati wa utume wa Nabii Ibrahim-Amani ya Mwenyezi Mungu Iwe Juu Yake-AS.  Alikuwa mwana wa Kanaani, ambaye alikuwa mwana wa Kushi, ambaye alikuwa mwana wa Sam (Shem), ambaye alikuwa mwana wa Nuhu (AS). Wengine wanaamini alikuwa mjukuu wa Hamu, mwana mwingine wa Nuhu (AS).

Nimrud alikuwa mfalme wa Babeli na kuna masimulizi tofauti kuhusu muda wa utawala wake, ambapo baadhi ya simulizi zinasema utawala wake ulidumu kwa miaka 400.

Moja ya hatua alizochukua ni kuamuru kuuawa kwa watoto wote waliozaliwa baada ya wanajimu kutabiri kwamba mvulana anayeitwa Ibrahim (AS) atazaliwa na atapigana na ibada ya sanamu. Pamoja na hayo, Ibrahim (AS) alizaliwa, akakua na kuwa kijana mwaminifu na anayeamini Mungu mmoja.

Nimrud alikuwa ameeneza ibada ya sanamu katika ufalme wake na kujiona kuwa mungu na mmiliki wa dunia. Inasemekana kwamba Nimrud alikuwa mtu wa kwanza kudai uungu.

Baada ya Ibrahim (AS) kuharibu masanamu na hivyo Nimrud alilenga kumwadhibu. Lakini kabla ya hapo, aliingia kwenye mjadala na Ibrahim (AS), ambao sehemu za mjadala huo zimetajwa katika Qur’ani Tukufu katika Sura Al-Baqarah:

“(Muhammad), Hukumwona yule aliye hojiana na Ibrahim juu ya Mola wake Mlezi kwa sababu Mwenyezi Mungu alimpa ufalme? Ibrahim alipo sema: Mola wangu ni yule ambaye huhuisha na kufisha. Yeye akasema: Mimi pia nahuisha na kufisha. Ibrahim akasema: Mwenyezi Mungu hulichomozesha jua mashariki, basi wewe lichomozeshe magharibi. Akafedheheka yule aliye kufuru; na Mwenyezi Mungu hawaongoi watu madhaalimu.” (Aya ya 258 ya Surat Al-Baqarah)

Mjadala huu umeelezwa kuwa ni aina ya makabiliano baina ya wema na uovu na uthabiti wa Tauhidi mbele ya ushirikina.

Baada ya kushindwa katika mdahalo huo, Nimrud aliamua kuwasha moto mkubwa na kumtupa Ibrahimu (AS) ndani yake lakini alikumbana na kushindwa katika hili pia kwa sababu Mungu aliufanya moto huo kuwa baridi na salama kwa Ibrahim (AS) na akaingia ndani ya moto kisha akatoka akiwa hajadhurika hata kidogo.

Baadaye, Nimrud alianza kile alichoona kuwa vita na Mwenyezi Mungu. Alifikiri kwamba Mungu yuko mbinguni, hivyo akajenga mnara mrefu ili kumfikia Mungu. Mnara huu, unaojulikana kama Mnara wa Babeli, uliharibiwa kwa amri ya  Mwenyezi Mungu.

Nimrud, ambaye alijiona kuwa na nguvu zaidi kuliko wote, aliuawa na mbu. Yule mdudu mdogo aliingia kwenye ubongo wa Nimrod na kumtia wazimu. Alikuwa na maumivu makali kiasi kwamba wengine walimpiga kichwani ili kumuua mbu. Halii hii iliendelea kwa siku arobaini na hatimaye kusababisha kifo chake.

captcha