IQNA

Qur’ani Tukufu Inasemaje /34

Mwenyezi Mungu hawapendi wakosaji au waanzao uadui

18:41 - November 14, 2022
Habari ID: 3476085
TEHRAN (IQNA) – Katika aya nyingi za Qur’ani Tukufu Mwenyezi Mungu anawaonya wale wanaovuka mipaka na kuwa na mawazo yenye misimamo mikali, kama vile katika Aya ya 190 ya Sura Al-Baqarah: “Kwani Mwenyezi Mungu hawapendi waanzao uadui.”

Katika jamii yoyote ile, kulingana na utamaduni, historia na imani yake, kuna makundi mbalimbali ya watu ambao wana tabia na mwenendo tofauti. Wakati mwingine kuna migogoro na mivutano kati ya makundi fulani. Kuhukumu juu ya nani aliye sahihi au mbaya au ni nani aliyeanzisha migogoro ni suala gumu lakini kuhusu jinsi mtu anapaswa kutenda na kutenda wakati kunapotokea mzozo, Qur'ani Tukufu haina mashaka katika kusisitiza haja ya kutovuka mipaka. “Na piganeni katika Njia ya Mwenyezi Mungu na wale wanao kupigeni, wala msianze uadui. Kwani Mwenyezi Mungu hawapendi waanzao uadui.” Surah Al-Baqara, Aya ya 190

Hii ni aya ya kwanza ya Qur’ani iliyoteremka kuhusu vita dhidi ya maadui wa Uislamu. Kuanzia hapo Mtukufu Mtume Muhammad (SAW) alipambana na wale walioanzisha vita dhidi ya Waislamu lakini si na wengine.  Kisha ilishuka aya ya 5 ya Sura At-Taubah: “Na ikisha miezi mitukufu basi wauweni washirikina popote mwakutapo, na washikeni na wazungukeni, na wavizieni katika kila njia….” Aya hii ilitoa ruhusa  ya kupambana na Mushrikeen.

Wafasiri wa Qur’ani Tukufu wametaja mambo fulani kuhusu aya ya 190 ya Sura Al-Baqarah. Imeamrisha kupigana na wale wanaowapiga vita Waislamu: “Na piganeni katika Njia ya Mwenyezi Mungu na wale wanao kupigeni…”. Maneno "kwa njia ya Mwenyezi Mungu" yanatoa mwanga juu ya lengo kuu la vita vya Kiislamu. Inadhihirisha kwamba vita katika mantiki ya Uislamu kamwe si kwa ajili ya kulipiza kisasi au matamanio au kujitanua au kupata nyara bali ni kwa ajili ya njia ya Mwenyezi Mungu. Lengo hili linaathiri nyanja zote za vita ikiwa ni pamoja na silaha gani zinaweza kutumika, jinsi ya kuamiliana na askari wa adui na wale waliokamatwa, nk.

Kisha Qur’ani Tukufu inaitaka kuwepo uadilifu hata katika medani ya vita na sio kuvuka mipaka: “Msiruke mipaka (msianze uadui), Kwani Mwenyezi Mungu hawapendi wapotovu (waanzao uadui).”

Wakati vita ni kwa ajili ya Mwenyezi  Mungu na katika njia ya Mwenyezi Mungu, lazima pasiwe na uvunjaji sheria na uchokozi. Ndiyo maana katika vita vya Kiislamu, tofauti na vita vinavyopiganwa sehemu mbalimbali za dunia hivi leo, kumekuwa na msisitizo mkubwa wa kuzingatia kanuni za kimaadili. Kwa mfano, ikiwa baadhi ya askari wa adui wataweka silaha zao chini au kuna wale ambao hawawezi tena kupigana au wale ambao hawakuweza kupigana mwanzoni mwa vita, kama vile waliojeruhiwa, wazee, wanawake na watoto, hawapaswi kushambuliwa. Aidha Uislamu unasema katika  vita mashamba na mazao yasiharibiwe na mabwawa ya maji ya kunywa yasiwe na sumu.

Hujjatul Islam  Mohsen Qara’ati katika tafsiri yake Qur’ani ya  Noor, anaashiria baadhi ya jumbe za aya na anasema:

1- Kutetea na kukabiliana na uchokozi ni haki ya binadamu. Mtu akipigana nasi tutapigana naye. "... wale wanaopigana nawe"

2- Katika Uislamu, lengo la kupigana si kuteka ardhi au ukoloni au kulipiza kisasi, bali ni kutetea ukweli au kuondoa makundi ya mafisadi na kuwaepusha watu na imani potofu na udanganyifu. “Katika njia ya Mwenyezi Mungu”

3- Uadilifu na haki vizingatiwe hata katika medani ya vita. “Usivuke mipaka”. Mara kwa mara Qur’ani Tukufu  imeonya kuhusu uasi na kuvuka mipaka.

4- Dhulma, ukosefu wa uadilifu, kuanzisha uadui  na kusimama dhidi ya dini ya Mwenyezi Mungu ni mambo ambao  lazima yaepukwe. “…Kwani Mwenyezi Mungu hawapendi waanzao uadui.”

6- Katika vita, lengo liwe tu sababu ya Mungu, sio matamanio, chuki, unafiki, n.k. “ Na piganeni katika Njia ya Mwenyezi Mungu na wale wanao kupigeni”

6- Hata katika kujitetea na kupigania haki, mtu anapaswa kumzingatia  Mwenyezi Mungu  kila wakati. Ingawa walianza vita dhidi yako na unapaswa kujitetea, ni lazima kujitetea kuwe ni kwa ajili ya Mungu. “Na piganeni katika Njia ya Mwenyezi Mungu.”

captcha