IQNA

Vita vya Saudia dhidi ya Yemen

Ujumbe kutoka Oman watembelea Yemen kuhuisha mapatano ya usitishaji vita

12:56 - December 22, 2022
Habari ID: 3476286
TEHRAN (IQNA) – Ujumbe kutoka Oman uko katika mji mkuu wa Yemen, Sana’a, kufanya mazungumzo na wanachama wa ngazi za juu wa harakati ya mapambano ya Kiislamu ya Ansarullah kuhusu kurefusha usitishaji vita unaosimamiwa na Umoja wa Mataifa nchini Yemen.

Muda wa kusitisha mapigano katika nchi hiyo maskini ya Kiarabu ulimalizika mapema Oktoba.

Mazungumzo hayo yanazingatia mipango na mapendekezo yaliyotolewa wakati wa mazungumzo na wawakilishi kutoka Saudi Arabia na wajumbe wa kimataifa. Hayo yamedokezwa na mkuu wa ujumbe wa kitaifa wa mazungumzo ya Yemen Mohammed Abdul-Salam.

Aidha amesema  muungano wa kivita unaoongozwa na Saudi Arabia ulilenga sekta ya uchumi ya Yemen na kuzua mgogoro mkubwa unaozidi kuongezeka nchini humo kwa njia ya vikwazo vikubwa dhidi ya benki vilivyosababisha kushuka kwa thamani ya sarafu ya taifa hilo.

Pindi maendeleo yatakapopatikana kuhusiana na kurejesha malipo ya mishahara kwa watumishi wote wa umma na kufunguliwa kwa viwanja vya ndege na bandari, masuala mengine yanaweza kujumuishwa katika mazungumzo ya amani pia, alidokeza.

Adbul-Salam pia alisisitiza kwamba masuala ya kibinadamu lazima yatenganishwe na masuala ya kisiasa na kijeshi, akisema kwamba matakwa ya harakati yake yanahusu Wayemeni wote, bila kujali rangi na asili yao.

"Muungano uvamizi unaoongozwa na Saudi Arabia unaelekea kutoa ahadi zisizo na maana kuhusu kurejelewa kwa mishahara ya umma, kuondolewa kwa mzingiro wa Yemen na kuondolewa kwa vikosi vya kijeshi vya kigeni," alisema.

Abdul-Salam alisifu juhudi za Oman za kurejesha amani na utulivu nchini Yemen, na kutoa usaidizi wa kibinadamu kwa Wayemeni ili kupunguza mateso yao, akibainisha kwamba ziara za mara kwa mara za wajumbe wa Oman huko Sana’a ni dalili za wazi za nia ya kusaidia ya Muscat.

Saudi Arabia ilianzisha vita vikali dhidi ya Yemen mwezi Machi 2015 kwa ushirikiano na washirika wake wa Kiarabu na kwa msaada wa silaha na vifaa kutoka Marekani na mataifa mengine ya Magharibi.

Lengo lilikuwa kuuweka tena utawala kibaraka wa Riyadh wa Abd Rabbuh Mansour Hadi na kuangamiza vuguvugu la Ansarullah, ambalo lina uungaji mkono mkubwa wa wananchi na limekuwa likiendesha masuala ya serikali bila ya kuwepo serikali inayofanya kazi nchini Yemen.

Wakati muungano unaoongozwa na Saudi Arabia umeshindwa kufikia malengo yake yoyote, vita hivyo vimeua mamia ya maelfu ya Wayemeni na kusababisha mgogoro mbaya zaidi wa kibinadamu duniani.

3481778

captcha