IQNA

Ansarullah ya Yemen: Wazayuni wanaendeleza ukatili wao huko Gaza bila huruma

18:13 - July 04, 2025
Habari ID: 3480891
IQNA – Kiongozi wa harakati ya mapambano ya Kiislamu ya Ansarullah nchini Yemen amelaani kuendelea kwa jinai za utawala wa Kizayuni dhidi ya raia wasio na hatia wa Palestina, huku jumuiya ya kimataifa ikikaa kimya bila kuchukua hatua yoyote.

"Adui dhalimu wa Kizayuni ameendelea kufanya mauaji ya halaiki dhidi ya watu wa Palestina huko Gaza kwa kipindi cha miezi 21, mbele ya macho ya Waislamu wa ulimwengu," alisema Abdul Malik Badreddin al-Houthi katika hotuba yake siku ya Alhamisi. "Adui huyo anaendeleza jinai kwa ukatili wa hali ya juu, kiasi kwamba hata wanyama wa mwituni wangesita kula nyama ya watu wa Gaza."

Aliongeza kuwa kadri damu ya watoto na wanawake wa Gaza inavyomwagika, ndivyo tamaa ya Kizayuni ya kuua na kufanya mauaji inavyoongezeka.

"Yanayofanywa na utawala huo ni kielelezo cha chuki, uadui, ukatili na jinai zake za muda mrefu," alisema al-Houthi. "Utawala haramu wa Kizayuni umekuwa ni genge linaloungwa mkono na Magharibi tangu mwanzo wake, kwa lengo la kuwatesa watu wa Palestina na Umma wa Kiislamu."

"Ni fedheha kubwa kwa taasisi za kimataifa, serikali na mataifa ambayo yananyamaza kimya mbele ya ukatili huu, huku watu wa Gaza wakisubiri msaada bila mafanikio."

Al-Houthi pia alikemea msaada wa Marekani kwa Israel, akisema kuwa kwa kutuma maelfu ya mabomu, Marekani inaendeleza jinai dhidi ya watu wa Palestina na Umma wa Kiislamu.

Kiongozi huyo alisisitiza kuwa marufuku ya usafiri wa majini wa utawala wa Kizayuni kutoka Yemen bado inaendelea kikamilifu katika Bahari Nyekundu, Bab el-Mandeb, Ghuba ya Aden na Bahari ya Kiarabu.

"Hatua hiyo ni sehemu ya mikakati pana ya muqawama dhidi ya njama za utawala wa Kizayuni na Marekani katika eneo hili," alieleza.

Alibainisha kwamba Ansarullah ilitekeleza mashambulizi 10 ya makombora na droni dhidi ya maeneo ya Kizayuni wiki hii, ikiwemo Yafa, Beersheba, Ashkelon na Umm al-Rashrash.

Aidha  al-Houthi, amezungumzia vita vya siku 12 vilivyoanzishwa na utawala wa Kizayuni wa Israel na washirika wake dhidi ya Iran na kusisisitiza kuwa "mfano wa Iran" umeonyesha kuwa nguvu ni matokeo ya muongozo wa Mwenyezi Mungu, uamuzi sahihi na ustahamilivu.

Kiongozi wa Mapinduzi ya Watu wa Yemen amesema: "Moja ya vipengee vikuu vya nguvu ya Iran ni kuwa thabiti katika misimamo yake. Badala ya kurudi nyuma au kufanya mapatano na adui, Wairani waliamua kutoa jibu madhubuti, na jibu hilo kali lilimlazimisha adui kusimamisha mashambuulizi yake licha ya misaada na uungaji mkono mkubwa wa Marekani na Magharibi."

Sayyid Abdul Malik amesema: "Israel haikuweza kuendelea na mashambulizi yake kutokana na gharama kubwa ilizolipa kutokana na uchokozi huo. Suala hili linadhihirisha wazi kwa Umma wa Kiislamu umuhimu wa kujiandaa kijeshi na kuwategemea wananchi."

Ametilia mkazo utayarifu kamili wa Iran kwa ajili ya jibu la kuangamiza zaidi iwapo Israel itafanya mashambulizi tena na kuongeza kuwa: Iran iko katika nafasi ambayo inaiwezesha kufanya mashambulizi makali zaidi kuliko hapo awali dhidi ya adui Mzayuni.

 

3493707

captcha