IQNA

Watetezi wa Palestina

Mufti wa Oman atoa wito wa kuwaunga mkono Mashujaa wa Yemen

20:53 - January 04, 2025
Habari ID: 3480002
IQNA – Mufti Mkuu wa Oman ametoa wito kwa mataifa yote kuwaunga mkono mashujaa wa Yemen ambao wanapigania haki na kupinga dhulma.

"Mashujaa wa Yemen wanaendelea kutetea haki zao na kupinga ukandamizaji na dhuluma kwa ushujaa usio na kifani na azma yenye nguvu ya kutosha kutikisa milima na kuvunja miamba," Sheikh Ahmed bin Hamad Al Khalili alisema katika taarifa, kwa mujibu wa tovuti ya Ray al-Yawm.

Ni muhimu kwa watu wote wenye ikhlasi Yemen kuungana ili kupata nguvu na kufikia malengo makubwa zaidi, alisema.

Zaidi ya hayo, ni muhimu kwa Ummah wote wa Kiislamu kuwaunga mkono, kwani ni haki ya Mwislamu mmoja juu ya mwingine, kama Mtume (SAW) alivyosema: “Muislamu ni ndugu wa Muislamu mwingine na wala hamdhulumu.

Sheikh al-Khalili aliendelea kusema kuwa lengo ambalo wapiganaji wa Yemen wanajitolea mhanga ni sababu ya mataifa yote.

Wayemen wananafanya kazi ya kuulinda mji mtakatifu wa Quds, ambao ni Kibla cha kwanza cha Waislamu na mahali ambapo Mtukufu Mtume (SAW) alipaa katika tukio la Mi’raj.

Tangu kuanza kwa kampeni ya mauaji ya kimbari ya utawala wa Israel katika Ukanda wa Gaza, wanajeshi wa Yemen wamechukua hatua za kuthibitisha uungaji mkono wao kwa  mapambano au muqawama wa Palestina huko Gaza, wakilenga meli za Israel katika Bahari Nyekundu na Lango Bahari la Bab el-Mandeb.

Zaidi ya hayo, wanajeshi wa Yemen wameanzisha mashambulizi kadhaa ya makombora na ndege zisizo na rubani dhidi ya maeneo yanayokaliwa na Israel, hasa Tel Aviv.

Kwa miaja mingi, Sheikh Ahmed bin Hamad Al Khalili amekuwa na msimamo imara katika uungaji mkono wake kwa ajili ya Palestina.

Vile vile amekosoa majaribio ya kuhalalisha uhusiano na utawala wa Israel na kupinga hatua yoyote ya Oman katika mwelekeo huo.

3491317

Habari zinazohusiana
captcha