IQNA

Mufti Mkuu wa Oman akemea Waarabu wanaotaka wapigania ukombozi wa Palestina wapokonywe silaha

15:11 - April 16, 2025
Habari ID: 3480550
IQNA – Kupitia taarifa kali kwenye mitandao ya kijamii, Mufti Mkuu wa Oman, Sheikh Ahmad bin Hamad Al-Khalili, amewakosoa vikali viongozi wa Kiarabu wanaoripotiwa kutoa wito wa kuwapokonya silaha wanamuqawama au wapigania ukombozi wa Palestina huko Gaza.

Akijibu hatua za hivi karibuni za kidiplomasia katika ukanda huo, hasa pendekezo la Misri kwa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina, Hamas, kuweka chini silaha zao, Al-Khalili amechapisha ujumbe kwenye X (zamani Twitter): "Uvamizi wa utawala wa Kizayuni dhidi ya Gaza na maeneo yote yaliyokaliwa kimabavu ya Palestina unaendelea bila kikomo—bila hata heshima kwa hospitali au maeneo yoyote ya hifadhi," aliandika.

Al-Khalili ameelezea hofu yake kuhusu mkinzano wa miito inayotolewa kwa makundi ya Wapalestina. “Ni miongoni mwa mkinzano wa ajabu kwamba wale wanaomiliki haki ndio wanaotakiwa kuweka chini silaha na wazikabidhi mkoloni—na cha kushangaza zaidi ni kwamba wito huu unatoka kwa ndugu zao Waarabu,” alisema.

Maoni yake yanaonekana kujibu moja kwa moja ripoti kuwa Misri, inayojaribu kupatanisha makubaliano ya kusitisha mapigano, imependekeza kujumuisha kuondolewa kwa silaha za makundi ya mapambano ya Palestina—hasa Hamas—kama sehemu ya makubaliano hayo. Hatua hiyo imekataliwa na Hamas, ambayo imetangaza kuwa silaha zao ni "msitari mwekundu" na hazihusiki katika mazungumzo.

Al-Khalili ameonya kuwa madai haya, yanayofanana na misimamo ya Israeli, yanaweza kudhoofisha harakati za Wapalestina. “Madai haya yanasaidia tu kuimarisha ukaliaji wa mabavu, kuongeza uvamizi, na kudhoofisha wanaosimamia ukweli,” alisema.

Mufti huyo alisisitiza kuwa mashambulizi dhidi ya Gaza bado yanaendelea bila kusita. “Uvamizi wa utawala wa Kizayuni dhidi ya watu wa Kiislamu wasiokuwa na ulinzi huko Gaza, na katika maeneo yote ya Palestina yaliyokaliwa kimabavu, unaendelea. Hawajali hata vituo vya afya, huduma za misaada, au sehemu za ibada,” aliongeza.

3492714

Habari zinazohusiana
captcha