IQNA

Jibu kwa jinai Israel

Mpalestina awaangamiza Wazayuni saba mjini Quds katika kulipiza kisasi

15:12 - January 28, 2023
Habari ID: 3476475
TEHRAN (IQNA)- Wazayuni saba waangamizwa Palestina kaskazini ya mji wa Al Quds (Jerusalem) unaokaliwa kwa mabavu na utawala dhalimu wa Israel.

Duru za habari zimeripoti usiku wa kuamkia leo kuwa, Wazayuni saba wameangamizwa kwa kupigwa risasi kaskazini mwa mji wa Al Quds unaokaliwa kwa mabavu.

Vyombo vya habari vya utawala haramu wa Kizayuni wa Israel imeripoti kuwa, walowezi saba wameangamizwa kufuatia ufyatuaji risasi uliotokea katika eneo la An-Nabiyyu-Yaaqub, lililoko kaskazini mwa Quds.

Vyanzo vya Kizayuni vimetangaza kuwa watu 12 walijeruhiwa pia katika shambulio hilo la ufyatuaji risasi.

Polisi wa Kizayuni wamemuua shahidi mmoja wa wahusika wa shambulio hilo huku wakiendelea kuwatafuta wahusika wengine.

Mpalestina Khayri Alqam anaaminika kuwa aliyetekeleza shambulio dhidi ya Wazayuni

Wazayuni hao saba wameangamizwa wakati siku ya Alkhamisi wanajeshi wa Kizayuni walishambulia kambi ya wakimbizi Wapalestina katika mji wa Jenin katika Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan ambako waliwaua shahidi Wapalestina kumi na kuwajeruhi wengine 20.

Katika kujibu jinai hiyo, vikosi vya muqawama wa Palestina vilifyatua makombora kadhaa kuelekea vitongoji vya walowezi wa Kizayuni.

Harakati za Muqawama za Palestina zikiwemo za Hamas na Jihadul-Islami zimepongeza operesheni ya kujitolea kufa shahidi ya Quds zikisisitiza kuwa hilo ni jibu la kutarajiwa kwa jinai za kinyama zinazofanywa kila uchao na utawala dhalimu wa Kizayuni wa Israel dhidi ya Wapalestina.

4117627

Kishikizo: wazayuni ، palestina
Jina:
Baruapepe:
* maoni:
captcha