IQNA

Qur'ani Tukufu

Wanafunzi wa Vyuo vya Kiislamu kutoka nchi 10 wanashiriki Mashindano ya Qur'ani ya Najaf

21:01 - January 19, 2025
Habari ID: 3480078
IQNA – Mashindano ya Kimataifa ya Qur'ani yanaendelea katika mji mtakatifu wa Najaf, Iraq, yakishirikisha wanafunzi wa Vyuo Vikuu vya Kiislamu (Hauza) au  seminari kutoka nchi 10 za Kiislamu.

Yameandaliwa na Kituo cha Qur'ani cha Najaf, kinachohusishwa na Mkutano wa Sayansi wa Qur'ani wa Idara ya Mfawidhi wa Haram ya Hadhrat Abbas (AS), kama ilivyoripotiwa na al-Kafeel.

Sayed Mohnad al-Miyali, mkurugenzi wa kituo hicho alisema mashindano ya kimataifa ya Qur'ani yamepangwa mahsusi kwa wanafunzi wa Hauza ya Najaf kutoka nchi mbalimbali.

Alisema yanalenga kuboresha ujuzi wao na ufahamu wa Qur'ani.

Katika hatua ya awali ya tathmini, kulikuwa na wanafunzi mia moja, 40 kati yao, ambao wanatoka nchi 10 za Kiislamu, walifikia hatua ya juu alisema.

Washiriki wanashindana katika makundi mbalimbali, ikiwa ni pamoja na kuhifadhi Juzuu 5, Juzuu 10, na Qur'ani yote, pamoja na katika maeneo ya tafakari na utafiti juu ya Qur'ani, afisa huyo alibainisha.

Aliendelea kusema kuwa mashindano hayo yanatoa fursa kwa wanafunzi wa seminari ya Najaf kuboresha maarifa yao ya Qur'ani kupitia ufahamu, tafakuri, na tafsiri ya Qur'ani, pamoja na kuimarisha ujuzi wao wa usomaji na Tajweed.

3491506

Habari zinazohusiana
captcha