IQNA

Qur'ani Tukufu katika maisha

Bwana Harusi mwenye ulemavu wa macho avutia wengi kwa usomaji Qur’ani Misri + Video

21:21 - February 02, 2023
Habari ID: 3476506
TEHRAN (IQNA)-Watumizi wa mitandao ya kijamii wanaendelea kusambaza video ya sherehe ya harusi ya wanandoa wa Misri, ambayo ilianza kwa bwana harusi mwenye ulemavu wa macho akisoma aya katika Sura Rum ya Qur'ani Tukufu.

Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, kitendo hiki cha bwana harusi mwenye ulemavu wa macho kiliwavutia wengi waliokuwepo kwenye sherehe hiyo. Baada ya kuswambazwa video hiyo, wanaharakati wa mitandao ya kijamii waliwapongeza wanandoa hawa wachanga na kutangaza kwamba jambo zuri zaidi ni kwamba bwana harusi ameanza maisha ya ndoa kwa kusoma aya za Qur'ani Tukufu.

Bwana harusi, ambaye jina lake ni Abdullah Mustafa, alisoma aya ya 21 na 22 za Surah Rum:

Na katika Ishara zake ni kuwa amekuumbieni wake zenu kutokana na nafsi zenu ili mpate utulivu kwao. Naye amejaalia mapenzi na huruma baina yenu. Hakika katika haya bila ya shaka zipo Ishara kwa watu wanao fikiri.  Na katika Ishara zake ni kuumba mbingu na ardhi, na kutafautiana ndimi zenu na rangi zenu. Hakika katika hayo zipo Ishara kwa wajuzi. 

Jina:
Baruapepe:
* maoni:
captcha