IQNA

Harakati za Qur'ani

Sherehe ya kuadhimisha miaka 40 Tangu kuanzishwa kwa Idhaa ya Qur'ani ya Iran

20:20 - February 11, 2023
Habari ID: 3476548
TEHRAN (IQNA) - Maadhimisho ya miaka 40 ya kuasisiwa Idhaa ya Qur'ani ya Iran yamefanyika katika hafla iliyofanyika hapa Tehran siku ya Ijumaa.

Idadi kadhaa ya walimu, wasomaji na wahifadhi wa Qur'ani Tukufu pamoja na mameneja na wafanyakazi wa Idhaa au Redio ya Qur'ani walihudhuria sherehe hiyo iliyorushwa moja kwa moja.

Mansour Qasrizadeh, mkurugenzi wa idhaa hiyo katika hotuba yake alibainisha kuwa Idhaa ya Qur'ani ilianzishwa tarehe 11 Februari 1983, katika mwaka wa tano wa ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu.

Alibainisha kuwa ilianzishwa kwa pendekezo la Ayatollah Sayed Ali Khamenei, ambaye alikuwa rais wa Iran wakati huo na ambaye sasa ni Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu.

Mwanzoni, Idhaa ya Qur’ani ilikuwa ikitangaza tu usomaji wa Qur'ani kwa saa chache kila siku lakini taratibu iliendeleza shughuli zake ili kujumuisha vipindi vya mafundisho ya Qur'ani na Kiislamu, aliongeza.

Katibu wa Baraza la Maendeleo ya Utamaduni wa Qur'ani la Iran Hujjatul Islam Hamid Mohammadi, Mjumbe wa Baraza la Wataalamu Mohammad Hossein Saffar Harandi, na Mojtaba Mohammadi, mkurugenzi wa Taasisi ya Qur'ani ya Meshakt, pia walihutubia katika hafla hiyo.

Idhaa ya Qur’ani inasimamiwa na Shirika la Utangazaji wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran (IRIB). Ni kituo cha redio kinachotangaza vipindi vya saa 24 kwa siku katika Lugha ya Kiajemi au Kifarsi.

Ceremony Marks 40th Anniversary of Iran Quran Radio Establishment   

Ceremony Marks 40th Anniversary of Iran Quran Radio Establishment   

Ceremony Marks 40th Anniversary of Iran Quran Radio Establishment   

Ceremony Marks 40th Anniversary of Iran Quran Radio Establishment   

4121243

captcha