Sheikh Shabib alikuwa miongoni mwa makari wanaoheshimiwa sana nchini Misri. Vitu hivyo vya thamani vitatayarishwa kwa ajili ya kuonyeshwa katika Makumbusho ya Makari wa Qur'ani, ambayo inatarajiwa kufunguliwa hivi karibuni.
Hatua hii ni sehemu ya mradi mpana wa Mamlaka ya Kitaifa ya Vyombo vya Habari ya Misri unaolenga kuweka kumbukumbu ya urithi wa maqari mashuhuri wa Qur’ani nchini humo, waliotambulika kwa sauti zao zilizogusa ulimwengu wa Kiislamu kwa kina.
Lengo kuu ni kuhakikisha kuwa mchango wao unaendelea kukumbukwa na vizazi vijavyo.
Awali, katika maandalizi ya uzinduzi wa makumbusho hayo, redio hiyo pia ilipokea turathi za Qari mashuhuri mwingine wa Misri, Sheikh Shaban El-Sayyad, katika hafla iliyohudhuriwa na maafisa wa vyombo vya habari pamoja na wataalamu wa Kimisri.
Sheikh Muhammad Ahmed Shabib alizaliwa tarehe 25 Agosti 1934 katika kijiji cha Dandit (Mit Ghamr, Mkoa wa Dakahlia). Alijiunga na Taasisi ya Zagazig ya Kufundisha Usomaji wa Qur'ani mwaka 1951. Jina lake lilianza kung’ara mwaka 1957 baada ya kusoma Qur’ani katika mazishi huko El-Mansoura pamoja na gwiji Sheikh Abdel Fattah El-Sha’shaei, jambo lililomthibitisha kama mmoja wa makari wakubwa wa Misri.
Mwaka 1961, alikumbwa na ugonjwa mbaya wa koo uliotishia kuharibu kabisa sauti yake, lakini kwa neema ya Mwenyezi Mungu alirejea tena na kupata mialiko ya kusoma Qur’ani kote nchini. Kufikia mwaka 1964, aliteuliwa rasmi kuwa msomaji wa Redio ya Qur’ani, na kujiunga na safu ya makari mashuhuri wa Misri.
Urithi wake unaakisi tukio la kihistoria la mwaka 1973 alipokuwa amealikwa na Yasser Arafat kusoma Qur’ani katika Msikiti wa Al-Aqsa, na akatuzwa kwa heshima ya kuitwa “Qari wa Msikiti wa Al-Aqsa.”
Sheikh Shabib alifariki dunia tarehe 3 Aprili 2012, akiwa ameacha urithi wa kiroho na sauti wa kudumu.
3493917