IQNA

Mwezi wa Ramadhani

Wauguzi Wasio Waislamu UAE wafunga Ramadhani katika mshikamano na wenzao Waislamu

14:29 - March 30, 2023
Habari ID: 3476785
TEHRAN (IQNA) – Wauguzi kadhaa wasio Waislamu katika Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) wanafunga kula na kunywa wakati wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani kwa vile wanataka kuonyesha mshikamano na wenzao Waislamu katika mwezi huu.

Kwa baadhi yao, hii ni mara ya kwanza watakuwa wanashiriki katika Saumu ya Mwezi Mtukufu wa Ramadhani wakati kwa wengine ni zoezi la kila mwaka. Pia kuna wauguzi ambao wanahisi kuwa mfungo wa mwaka huu ni maalum kwani Ramadhani imesadifiana na wakati ambapo Wakristo wengi pia huzingatia kufunga au kuacha starehe.

Wauguzi hao wanasema kwamba kufunga wakati wa mwezi mtukufu wa Ramadhani imekuwa sehemu ya maisha yao na wamegundua faida kadhaa za kiafya kutokana na kufunga.

Shoba Varughese, Mkurugenzi Msaidizi wa Hospitali ya Nursing Medeor, Dubai ni mmoja wa wauguzi wanaofunga mfungo wa mwezi wa Ramadhani. “Zaidi ya wenzetu 20 wanafunga katika mwezi mtukufu. Wenzetu wasio Waislamu wanawaunga mkono waliofunga. Ninajaribu kufunga siku nyingi iwezekanavyo kila mwaka, "alisema Varghese.

“Kumaliza mfungo na wenzetu kunatupa hisia za kipekee. Umoja na kuheshimiana ni maadili ambayo nchi yetu inakuza, na tunafurahi kuona hilo katika mwezi mtukufu, "aliongeza.

Mwenzake Varghese, George Bautista, huwa anausubiri kwa kwa hamu mwezi mtukufu wa Ramadhani. "Ninafunga wakati wa Ramadhani ili kushikamana na Waislamu  karibu nami. Nina marafiki wengi Waislamu. Huwa nasubiri kwa hamu futari na kuungana nao," Bautista alisema.

Jisha Kurian, muuguzi katika Hospitali ya Aster, Qusais, amekuwa akizingatia kufunga wakati wa Ramadhani kwa miaka sita iliyopita. Alitiwa moyo na mmoja wa wazee wake ambaye alikuwa akifunga ingawa hakuwa Mwislamu. "Ni ngumu kufanya kazi wakati wa kufunga, lakini sioni ni vizuri kutumia chakula au maji wakati wenzangu Waislamu wanafanya kazi huku wakiwa katika Saumu ya Ramadhani. Kwa hivyo, mimi pia hujiunga nao na hujumuika nao wakati wa Ifar," Kurain alisema.

"Kufunga hufanya akili yangu kuwa na nguvu na kunipa uwazi wa mawazo yangu. Inasafisha akili zetu na kuleta hali chanya, "aliongeza.

Kwa Jaisy Joseph, anayefanya kazi katika Hospitali ya Medeor, kufunga si jambo geni. Akiwa ameishi Saudi Arabia, alianza kufunga pamoja na Waislamu wenzake huko. "Nimekuwa nikiadhimisha mwezi mtukufu pamoja na Waislamu wenzangu hapo awali, hata hivyo, hii ni Ramadhani yangu ya kwanza katika UAE. Mwaka huu, ni maalum zaidi kwa sababu Ramadhani inasadifiana na Kwaresima, kipindi cha kila mwaka ambacho Wakristo husali na kufunga kwa ajili ya maandalizi ya Pasaka. Kufunga hutuleta pamoja kama familia na kuimarisha uhusiano wetu,” alisema Joseph.

Mwenzake Kurian Pretty Mathew, kutoka idara ya magonjwa ya wanawake, amekuwa akifunga kwa miaka mitatu. "Idara yetu katika hospitali ina shughuli nyingi mwaka mzima. Wafanyakazi wenzangu Waislamu hufunga na kufanya kazi. Kwa hiyo, miaka mitatu iliyopita, nilijiunga nao katika kufunga wakati wa mwezi mtukufu. Sikuwa na uhakika kama ningeweza kutimiza lakini nilifanikiwa na imekuwa uzoefu wa ajabu kwangu. Sioni ugumu kufanya kazi ninapokuwa nimefunga. Ninahisi Mungu anatupa nguvu tunapofunga,” Mathew alieleza.

Mwenzake Joseph, Nazeera Syed, mkurugenzi wa uuguzi katika hospitali hiyo, anasema, "Nimeshuhudia kugawana majukumu katika sehemu zetu za kazi. Wenzetu wasiofunga watajitokeza kusaidia wale wanaofunga na kuchukua kazi ya ziada. Kutokuwa na ubinafsi na kusaidiana ni maadili tunayoshikilia na kusherehekea kila wakati," Syed alisema.

3482992

captcha