IQNA

Kiongozi wa Ansarullah

Wanovunjia heshima Qur'ani Tukufu wawekewe vikwazo

16:06 - March 31, 2023
Habari ID: 3476789
TEHRAN (IQNA)- Kiongozi wa harakati ya wananchi ya Ansarullah ya Yemen amesema kuwa, watu wanaoongoza jinai ya kuvunjia heshima matukufu ya Kiislamu na kulikariri hilo ni lobi za Wazayuni.

Sayyid Abdul-Malik Badruldeen al-Houthi amesema hayo katika hotuba yake ya mwezi mtukufu wa Ramadhani na kulaani vikali vitendo vya mara kwa mara vya kuvunjiwa heshima Qur'ani Tukufu na matukufu mengine ya Kiislamu.

Kiongozi huyo wa Ansarullah ya Yemen amesisitiza kwa kusema: Kushikamana kwetu na dini na itikadi yetu ya Uislamu ni jambo ambalo linatutaka tuwe na hasira na ghadhabu pindi dini yetu inapovunjiwa heshima.

Sayyid Abdul-Malik Badruldeen al-Houthi ameashiria mfungamano wa maadui na ulimwengu wa maada na kupenda dunia na kueleza kwamba, Umma wa Kiislamu unapaswa kutumia silaha ya vikwazo vya kiuchumi kupambana na maadui wa dini yao kwani uchumi ni sanamu linaloabudiwa na maadui.

Amesema mataifa ya Kiislamu yanapaswa kuyawekea vikwazo vya kiuchumi madola yanayovunjia heshima matukufu ya Kiislamu na kulitumia hilo kama silaha ya kumfanya adui asikariri vitendo hivyo,

Siku chache zilizopita, kundi lenye chuki dhidi ya Uislamu la Patrioterne Gar Live, lilichoma moto nakala ya Qur'ani Tukufu huko Copenhagen, mji mkuu wa Denmark.

Aidha mapema mwaka huu, Rasmus Paludan, mwanasiasa mwenye misimamo mikali wa Denmark alichoma moto nakala ya Qur'ani Tukufu karibu na Ubalozi wa Uturuki mjini Stockholm huku akiwa analindwa na polisi ya Sweden.

Kadhalika Edwin Wagensveld, mwanasiasa mwingine wa siasa kali za mrengo wa kulia wa Uholanzi, na kiongozi wa kundi la chuki dhidi ya Uislamu la Pegida, alirarua kurasa za Qur’ani Tukufu huko The Hague, mji mkuu wa Uholanzi. Video ya Wagensveld kwenye Twitter ilionyesha kuwa alichoma kurasa zilizochanwa za Qur’ani Tukufu.

 

4130674

captcha