IQNA

Imam Khomeini

'Mtazamo wa Imam Khomeini kuhusu Suala la Palestina Ulitokana na Utambuzi wa Qur'ani Tukufu

11:20 - June 03, 2023
Habari ID: 3477086
TEHRAN (IQNA)- Mwanachama wa ngazi ya juu wa harakati ya Jihad ya Kiislamu ya Palestina amesema mtazamo wa kina wa Imam Khomeini (AS) kuhusu suala la Palestina ulitokana na utambuzi wake wa Qur'ani na kidini.

Ramiz al-Halabi alisema hayo alipokuwa akihutubia katika semina ya kimataifa iliyopewa jina la “Mtazamo wa Imamu Khomeini Kuhusu Tauhidi na Maadili katika Ulimwengu wa Sasa; Mafanikio na Mtazamo wa Baadaye”.

Kongamano hilo Ilifanyika siku ya Ijumaa, kabla ya Hauli ya Miaka 34 ya Kuaga Dunia muasisi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.

Katika hotuba yake Al-Halabi amezungumzia fikra za Imam Khomeini na mwamko wa Kiislamu na binadamu wa zama hizi kwa kuzingatia suala la Palestina.

Amesema Imam Khomeini (RA) alikuwa mwanazuoni mkubwa ambaye aliyatazama masuala ya ulimwengu wa Kiislamu kwa mtazamo wa Uislamu na alikuwa na mtazamo mpana, wa kistaarabu na wa umoja kuhusu Umma wa Kiislamu.

Imam Khomeini aliliunga mkono taifa lililokandamizwa la Palestina kwa kuwa alikuwa ni Mwislamu ni Mwislamu wa madhehebu ya Shia wakati aghalabu ya Wapalestina ni Waislamu wa madhehebu ya Wasunni, alisema. Al-Halabi ameongeza kuwa, Imam Khomeini alilichukulia suala la Palestina kuwa suala la kimsingi na la kistratijia la ulimwengu wa Kiislamu.

Amebainisha kuwa Imam Khomeini (RA) hakuacha juhudi zozote katika kuliunga mkono taifa na mapambano ya Palestina bila ya kujali misimamo yao ya kisiasa.

Bila shaka, alisema, Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran na uongozi wake daima umekuwa ukiunga mkono mapambano yote ya watu wanaodhulumiwa dhidi na madola ya kibeberu lakini Palestina imekuwa na nafasi maalum.

Al-Halabi aliendelea kueleza imani yake kwamba bendera za ukweli hivi karibuni zitapandishwa katika ulimwengu wote wa Kiislamu, ikiwa ni pamoja na katika Msikiti wa Al-Aqsa, na wafuasi na waumini wa Imam Khomeini katika siku za usoni.

Semina hiyo iliandaliwa na makao makuu kwa ajili ya kufanya sherehe za kuadhimisha miaka 34 ya kufariki kwa Imam Khomeini kwa ushirikiano na kituo cha utafiti cha Imam Khomeini na Mapinduzi ya Kiislamu na idara ya kimataifa ya Taasisi ya Kukusanya na Kuchapisha kazi za Imam Khomeini.

Wasomi na wanafikra kutoka Iran, Lebanon, Palestina, Uzbekistan, Japan, Iraq, Ujerumani, Malaysia na Romania walihutubia semina hiyo.

4145069

captcha