IQNA

Kiongozi wa Hizbullah: Misingi ya Imam Khomeini (MA) itasalia kuwa nuru ya Muqawama

13:54 - June 02, 2025
Habari ID: 3480775
IQNA-Katibu Mkuu wa Hizbullah ya Lebanon, Sheikh Naeem Qassem, amesisitiza kuwa mafundisho Uislamu asili wa Mtume Muhammad kupitia misingi ya kimapinduzi ya Imam Ruhollah Khomeini (Mwenyezi Mungu Amrehemu) yataendelea kuwa mwanga unaoongoza harakati za mapambano au Muqawama na vuguvugu za ukombozi katika eneo la Asia na ulimwengu mzima wa Kiislamu.

Katika taarifa aliyotoa kwa mnasaba wa kuwadia kumbukumbu ya mwaka 36 tokea alipoaga dunia Imam Khomeini (MA), Sheikh Qassem amesema kuwa: "Imam Khomeini aliibadilisha Iran kutoka taifa lililokandamizwa na utawala wa kidikteta unaoungwa mkono na Marekani, na kuifanya kuwa nchi inayosimama imara pamoja na wanyonge duniani."

Sheikh Qassem amesema kuwa kupitia harakati yake ya kimapinduzi, Imam Khomeini alidhihirisha kwa vitendo Uislamu halisi wa Mtume Muhammad (SAW), na leo hii, taifa la Kiislamu linaishi chini ya mwanga wa mafundisho hayo.

"Fikra ya Imam Khomeini bado imesimama imara," alisema Sheikh Qassem. "Imam alikuwa mfano wa uadilifu wa kiimani; alikataa wazi wazi dhulma, uvamizi na ukoloni. Misingi hiyo imeendelea kuwa dira ya harakati za muqawama (mapambano) na vuguvugu zote za ukombozi katika eneo hili."

Amesisitiza nafasi ya Iran ya Kiislamu, Sheikh Qassem alisema: "Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, chini ya uongozi wa Imam Khomeini, imesimam kidete kando ya harakati za mapambano ya ukombozi wa Palestina na Quds tukufu. Iran ina nafasi ya kipekee katika kusimamia na kuunga mkono malengo ya umma wa Kiislamu."

Sheikh Qassem amehitimisha kwa kusema kuwa mafanikio ya Imam Khomeini yamewawezesha wafuasi wa haki kuishi kwa matumaini, wakiamini kuwa “mwisho wa dhulma uko karibu na ushindi wa haki dhidi ya batili hauepukiki.”

 

3493305

Habari zinazohusiana
captcha