IQNA

Rekodi mpya ya waliosilimu Kuwait katika Mwezi wa Ramadhani

14:40 - April 04, 2025
Habari ID: 3480493
IQNA – Katika mwezi Mtukufu wa Ramadhani wa mwaka 1446 Hijria (2025) , Kuwait imesema imeshuhudia ongezeko la ajabu la watu wanaokumbatia Uislamu.

Ammar Al-Kandari, Mkurugenzi Mkuu wa Kamati ya Kuarifisha Uislamu, ametangaza kuwa kufikia siku ya 29 ya mwezi mtukufu wa Ramadhani mwaka huu, takriban watu 730, wakiwemo wanaume na wanawake kutoka mataifa mbalimbali, walikuwa wamesilimu au wameingia katika dini ya Kiislamu.

Takwimu hii inaashiria idadi kubwa zaidi ya watu waliokubali Uislamu maishani kuwahi kurekodiwa katika kipindi cha miaka saba iliyopita.

Al-Kandari alihusisha mafanikio haya na neema ya Mwenyezi Mungu pamoja na juhudi zisizo na kikomo za wahubiri 78 wa kiume na wa kike waliojitolea kikamilifu kwa ajili ya kazi hii muhimu.

Amesisitiza mchango wa kampeni ya “Badilisha Maisha Yao” iliyoanzishwa na kamati hiyo, katika kuwaeleza wasiokuwa Waislamu mafundisho ya Uislamu wakati wa Ramadhani.

Kampeni hiyo inaripotiwa kuhusisha shughuli mbalimbali za kueneza uelewa, kama mihadhara na usambazaji vitabu n.k.

Kumekuwa na ongezeko la watu wanaokumbatia Uislamu duniani kote tangu kuanza kwa vita vya utawala wa Israel dhidi ya Gaza mwezi Oktoba 2023.

 

3492559

Kishikizo: kuwait ramadhani silimu
captcha