IQNA

16:49 - February 15, 2020
News ID: 3472473
TEHRAN (IQNA) – Msikiti uliojengwa miaka 130 iliyiopita nchini Singapore, umefunguliwa baada ya ukarabati wa miaka miwili na sasa unaweza kubeba waumini 2,500 kutoka 1,500.

Baada ya ukarabati, msikiti huo una lifti, ukumbi maalumu kwa ajili ya wanawake, vyumba vya darasa, ukumbi unaoweza kutumika kwa ajili ya shughuli mbali mbali na shuhula zingine kwa ajili ya jamii ya Waislamu.

Ukarabati wa msikiti huo unaojulikana kama Masjid Angullia umegharimu dola za Kimarekani milioni 6.3 na umekarabatiwa katika mpango wa ukarabati wa misikiti unaotekelezwa na Baraza la Kiislamu la Singapore.

Msikiti huo umefunguliwa rasmi na waziri anayesimamia masuala ya Waislamu nchini Singapore, Masago Zulkifli.

Msikiti huo ulijengwa kwa mara ya kwanza mwaka 1890 na mfanya biashara Mohammad Salleh Eusoff Angulia, ambaye alikuwa Muislamu wa madhehebu ya Sunni kutoka Gujarat nchini India na hivi sasa unasimamiwa na mjukuu wake, Ayoob Angullia.

Msikiti wa Angullia hutumiwa sana na wafanyakazi wa kigeni, hasa siku za wikiendi na pia katika siku maalumu hasa Idul Fitri na Idul Adha.

Akizungumza wakati wa ufunguzi, Ayooba alitoa wito kwa Waislamu kutumia fursa iliyojitokeza kwa kujifunza Uislamu katika msikiti huo uliokarabatiwa.

Singapore au Singapuri ni nchi ndogo na iliyostawi katika Asia ya Kusini-Mashariki ambayo uchumi wake unategemea zaidi biashara, hasa benki pamoja na viwanda. Waislamu wanakadiriwa kuwa asilimia 15 ya watu wote milioni 5.6.

Msikiti wa kihistoria wa wafunguliwa Singapore baada ya ukarabati wa dola milioni 6.3

Msikiti wa kihistoria wa wafunguliwa Singapore baada ya ukarabati wa dola milioni 6.3

Msikiti wa kihistoria wa wafunguliwa Singapore baada ya ukarabati wa dola milioni 6.3

3878785

Name:
Email:
* Comment:
* captcha: