IQNA

Watetezi wa Palestina

Maandamano dhidi ya kuunga mkono Palestina yaendelea huku Israel ikishadidisha jinai

13:47 - December 11, 2023
Habari ID: 3478018
IQNA - Maandamano duniani kote kupinga na kulaania mauaji ya kimbari yanayotekeleza na utawala haramu wa Israel kwa himaya ya Marekani dhidi ya Wapalestina huko Gaza yanaendelea duniani kote.

Nchini Indonesia, maelfu ya watu walifanya maandamano ya kuunga mkono Palestina huko Medan, kwa matumaini kwamba usitishwaji wa mapigano ungetokea katika Ukanda wa Gaza hivi karibuni.

Nchini Uturuki, maandamano ya wakati mmoja nchini kote yalishuhudia maelfu ya watu wakielezea hasira zao kwa Israeli kwa uhalifu dhidi ya ubinadamu huko Gaza.

Waandamanaji nchini Marekani wamekusanyika mbele ya nyumba ya Waziri wa Mambo ya Nje wakilalamikia uungaji mkono wake kwa utawala wa Kizayuni dhidi ya watu wa Gaza.

Anthony Blinken Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani amekuwa akitoa matamshi ya mara kwa mara akiunga mkono jinai za utawala wa Kizayuni huko Gaza na kujaribu kuwaonyesha walimwengu kuwa Wazayuni ni wahanga walio na haki ya kujilinda.

Ijumaa kundi la waandamanaji wanaounga mkono Palestina walikusanyika mbele ya nyumba ya Anthony Blinken huko Washingtone na kumtuhumu kwa kuunga mkono mauaji ya kimbari ya Wazayuni dhidi ya Wapalestina.

Waandamanaji walipiga nara dhidi yake akiwa anatoka nyumbani kwake mjini humo. 

Huku wakipeperusha bendera wakiwa wamevalia hafia za Kipalestina waandamanaji hao pia wametaka kusimamishwa misaada ya kijeshi ya Marekani kwa Israel.

Waandamanaji hao dhidi ya Wazayuni wamesisitiza umuhimu wa kukomeshwa vita na kudumishwa amani katika Ukanda wa Gaza.

Uungaji mkono wa Marekani kwa utawala wa Kizayuni unapelekea kushadidi siku baada ya siku jinai za utawala huo katika ukanda huo.

Ijumaa, ikiwa ni katika moja ya hatua zake za upendeleo kwa Israel dhidi ya wananchi wa Gaza, Marekani ilipinga kwa kura ya veto, azimio lililopendekezwa na Umoja wa Falme za Kiarabu kwa ajili ya usitishaji vita katika Ukanda wa Gaza.

Tangu yalipoanza kushuhudiwa matukio ya hivi sasa kwenye eneo la Asia Magharibi hasa baada ya tarehe 7 Oktoba, kufuatia operesheni ya kishujaa ya #Kimbunga_cha_al-Aqsa iliyoongozwa na Harakati ya Mapambano ya Palestina HAMAS dhidi ya utawala wa Kizayuni wa Israel, madola ya kibeberu yamezidi kuonesha uungaji mkono wao kwa jinai za Israel.

Zaidi ya miezi miwili nyuma, utawala katili wa Kizayuni ulianza kuua kinyama raia, watoto wachanga, watoto wadogo, wanawake, vizee na raia wa kawaida wa Ghaza baada ya kushindwa kukabiliana na wanamapambano wa Palestina kwenye medani za vita. Nchi za Magharibi zikiongozwa na Marekani, Uingereza na Canada zimekuwa zikishiriki moja kwa moja kwenye jinai hizo za Wazayuni ambazo hadi hivi sasa zimeshaua shahidi zaidi ya Wapalestina 17,700 wengi wao wakiwa ni wanawake na watoto wadogo.

/3486371

Habari zinazohusiana
captcha